Pages

NMB Bank yaja kivingine, Sasa unaweza kujifungulia akaunti popote pale

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi wa bidhaa mpya za benki hiyo, ikiwemo na ile ya mteja kwa simu yake kujifungulia akaunti popote alipo.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Benard Kibesse (kushoto) na mgeni rasmi katika uzinduzi wa bidhaa mpya za NMB, akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi wa bidhaa hiyo ya NMB leo jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wageni waalikwa wakishuhudia hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya za Benki ya NMB leo jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya wageni waalikwa wakijaribu huduma za NMB kwa kutumia simu zao.

Baadhi ya wageni waalikwa wakishuhudia hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya za Benki ya NMB leo jijini Dar es Salaam.

BENKI ya NMB sasa imeendelea kuboresha huduma za kibenki nchini hasa kuvutia kila raia kumiliki akaunti ya benki kwa matumizi mbalimbali katika shughuli za kila siku. Ili kuhakikisha suala hilo linatekelezeka, NMB imekuja na huduma iliyoboreshwa zaidi nay a kisasa ambapo kila Mtanzania anaweza kujifungulia akaunti yake kupitia simu yake ya mkononi aina yoyote ile.

Akizinduwa huduma hiyo leo jijini Dar es Salaam, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Benard Kibesse ameipongeza Benki ya NMB kwa kuwa wabunifu wa kutumia teknolojia ambayo inachochea wananchi kutolazimika kutembea na fedha wakati wote kwenye mahitaji yao.

Alisema utaratibu wa watu kutembea na fedha mfukoni kwa ajili ya matumizi unapitwa na wakati na nihatari kwa usalama wa mtu na fedha zake hivyo kuna kila sababu ya kuja na suluhisho kama la NMB.

Awali akifafanua juu ya huduma hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker alisema kwa sasa bila kujali aina ya simu anayotumia Mtanzania, anaweza kujifungulia akaunti yake akiwa nyumbani au popote pale kwa kutumia simu yake.

Alisema huduma ya kujifungulia akaunti hiyo ni rahisi na inaweza kukamilika ndani ya dakika tatu kisha unapata akaunti yako huku namba yako ya simu ikiwa ndio namba ya akaunti hiyo. Alisema huduma hiyo inaweza pia kufanyika kwa kutumia NMB Klik App kwa wenye simu janja (smart phone).

Alisema NMB inakuwa ni benki ya kwanza kutoa huduma ya mteja kujifungulia akaunti yake pasipo kutembelea tawi la benki au kuitaji mlolongo wa makaratasi. Anasema mara baada ya kuwa na akaunti hiyo mteja anaweza kuanza kuitumia papo hapo kwa shughuli zote za kibenki bila makato ya kila mwezi.

“…Lengo la NMB ni kumfikia kila Mtanzania na kumpa huduma za kibenki ili kumuingia katika mfumo rasmi wa kiuchumi na maendeleo. Kuingia kwenye huduma hii mteja anatakiwa kupiga *150*66# au ku-pakuwa NMB Klik App (Google Play au App Store) kwa wateja wa simu janja kisha kuanza kujihudumia…,” alisema Bi. Bussemaker katika uzinduzi huo.

Aliongeza ndani ya huduma hizo mteja anaweza kufanya huduma mbalimbali kwa kutumia simu na NMB Klik App kama vile, kupata mkopo, kulima bili anuai, kufanya malipo ya manunuzi mbalimbali nje na ndani, kuwekeza fedha na kupata faida, malipo ya fedha za kigeni na hata kufanya mahesabu na miamala ya kifedha.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)