BENKI YA NMB YAZIPIGA JEKI SHULE ZA MSINGI NA HOSPITALI NCHINI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BENKI YA NMB YAZIPIGA JEKI SHULE ZA MSINGI NA HOSPITALI NCHINI

Meneja wa NMB tawi la Muhimbili - Happiness Mengi akikabidhi sehemu ya mashuka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) - Dk Respicious Boniface kama mchango wa benki kwa jamii. Jumla ya mashuka 172 yenye thamani ya shilingi milioni 5 yalikabidhiwa na benki ya NMB kwenye hafla iliyofanyika katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Fedha na Ugavi, Kelvin Felix, Mkurugenzi wa Tiba wa  Muhimbili - Dk Samuel  Swai na Meneja wa tawi la NMB Muhimbili wakiwa wameshika mashuka yaliyotolewa na benki hiyo kwa Taasisi ya MOI.

Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma - Dr Omari Nkullo (kushoto) akipokea msaada wa mabati 250 kutoka kwa Meneja wa Nmb Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi (kulia) kwa ajili ya kuezekea vyumba vya madara vya shule ya Msingi Songambele iliyopo Wilayani Kongwa. katikati ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo - Robert Rutairwa,msaada wa mabati hayo unathamani ya sh. milioni 5.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Songambele Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma wakihamisha mabati yaliyotolewa na Benki ya Nmb kwa ajili ya kuezekea vyumba vya madarasa shuleni hapo.

Meneja Mahusiano, Biashara za Serikali wa benki ya NMB kanda ya Mashariki – Aneth Kwayu akimkabidhi madawati Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe - Jokate Mwegelo yaliyotolewa na benki ya NMB.

Misaada mbalimbali iliyotolewa na Benki ya NMB ikikabidhiwa kwa wahusika

Misaada mbalimbali iliyotolewa na Benki ya NMB ikikabidhiwa kwa wahusika

BENKI ya NMB imetoa msaada wa madawati 100 kwa shule za msingi mbili, vifaa vya ujenzi na vifaa vya hospitali vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 25 katika Mikoa ya Pwani, Dodoma na Dar es Salaam.

Benki hiyo imetoa Madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa shule za msingi Masaki ya wilayani Kisarawe Mkoani Pwani na Shule ya Msingi Msimbazi Mseto za jijini Dar es Salaam.

Msaada Mwingine uliotolewa ni Mashuka kwaajili ya taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili – Moi ya Jijini Dar es Dalaam yenye thamani ya shilingi Milioni Tano, Magodoro na vitanda vya wajawazito kwa hospitali ya wilaya ya Kongwa vyenye thamani ya shilingi Milioni tano na vifaa vya ujenzi kwaajili ya shule ya msingi Songambele yenye thamani ya shilingi Milioni tano hivyo kufanya msaada wote kuwa wa shilingi Milioni 25.

Hata hivyo, huu ni mwendelezo wa benki kujali wateja na jamii inayozunguka matawi yake huku ikiamini kuwa ni kupitia jamii ndipo wateja wake wengi wanapotoka, kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni utamaduni waliojiwekea.

Kwa mwaka huu – 2018, Benki ya NMB imepanga kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni 1 kusaidia jamii katika Nyanja za elimu na afya pamoja na kusaidia vipaumbele vilivyowekwa na serikali kwenye elimu ikiwa ni pamoja na Tehama na maabara kwa shule za msingi na sekondari.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages