AIRTEL NA WADAU WATOA TIBA NA UCHUNGUZI WA AFYA YA KINYWA NA MENO BURE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

AIRTEL NA WADAU WATOA TIBA NA UCHUNGUZI WA AFYA YA KINYWA NA MENO BURE

Wakwanza kulia ni Mtoa huduma wa kutuo cha tiba ya Kinywa na Meno cha Elite Dental Clinic Bi Baby Luck akiwa na Muuguzi wa Kituo hicho Bi Rosemary Kwilasa wakitoa ushauri wa tiba ya meno kwa wafanyakazi wa Airtel kutoka vitengo mbalimbali pamoja na wadau wao. Airtel imefanya Gulio maalum la kuwakutanisha wadau na watoa huduma mbalimbali pamoja na wafanyakazi wake kupata huduma hizo BURE. Gulio hilo Gulio lililofanyika makao makuu ya Airtel.
Dokta Latha Sujit (kushoto) wa Elite Dental Clinic akiwa na Muuguzi wa Kituo hicho wakitoa ushauri wa tiba ya meno kwa mfanyakazi wa Airtel Bw James Moilo kutoka vitengo mauzo wakati Airtel ilipofanya Gulio maalum la kuwakutanisha wadau na watoa huduma mbalimbali pamoja na wafanyakazi wake kupata huduma mbalimbali BURE. Gulio hilo lililofanyika makao makuu ya Airtel.
Meneja Mauzo na Masoko wa Seifi Group Bi Zarina Riyas (mwenye baibui) akiwa na watoa huduma wengine wa kampuni hiyo wakitoa huduma kwa mfanyakazi wa Airtel wakati Airtel wa ilipofanya Gulio maalum la kuwakutanisha watoa huduma mbalimbali pamoja na wafanyakazi wake kupata huduma hizo BURE. Gulio hilo lililofanyika makao makuu ya Airtel.


Dokta Latha Sujit (kushoto) wa Elite Dental Clinic akiwa na Muuguzi wa Kituo hicho wakitoa ushauri na tiba ya meno kwa mdau wa habari mtandaoni wa Michuzi media Group Bw Ahmadi Michuzi wakati Airtel ilipofanya Gulio maalum la wadau na wafanyakazi wake kukutana na watoa huduma mbalimbali nakupata huduma mbalimbali BURE. Gulio hilo lilifanyika makao makuu ya Airtel.
Meneja Masoko wa Club9 inayojiusisha na huduma ya Mazoezi tiba Bi Janeth John akiwa na watoa huduma wengine wa kampuni hiyo wakitoa huduma kwa mmoja ya mdau wa Airtel kwenye Gulio maalum la watoa huduma mbalimbali BURE. Gulio hilo lilifanyika makao makuu ya Airtel.

Airtel yawezesha uchunguzi wa afya na matibabu BURE kwa wadau na wafanyakazi wao
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imeungana na wadau wengine kutoa tiba na uchunguzi wa afya ya kinywa na meno bure ikiwa ni juhudi zake za kutambua umuhimu wa Afya ya Kinywa na Macho. Uchunguzi huo imefanyika kwenye makao makuu ya Airtel na kuwafaidisha wafanyakazi kutoka vitengo mbali mbali pamoja na wadau wengine waliofika kwenye ofisi za kampuni hiyo.

Akiongea wakati wa tukio hilo Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu Airtel Bi Stella Kibacha alisema “Airtel Tanzania tunatambua watu walio kwenye ajira mbalimbali hubanwa sana na kazi na wakati mwingine kukosa muda wa kuchunguza mwenendo wa Afya zao, hii ndio imetufanya Airtel kuwaleta wadau wetu hapa ili wafanyakazi wetu pamoja na wadau wanaotembelea jengo la Airtel kupata huduma hizi”

Kibacha aliendelea kueleza kuwa kuwa “wote tunatambua Wizara ya Afya kupitia waziri Ummy Mwalimu imekuwa mstari wa mbele kusisitiza sana swala la kulinda Afya zetu, sisi Airtel tumeona umuhimu wake pia ndio maana watoa huduma wa Afya ya kinywa Elite wapo, Macho wapo wadau wetu International Eye Hospital na Mazoezi tumewaita Club9 Wellness Servicess kuja hapa na wataalam wao ili kutoa ushauri wao kwa jamii hapa ofisini kwetu kwa siku nzima wafanyakazi na wadau wakaribu wapate muda wa kufanyiwa uchunguzi wa awali na kupanga muda wao kwenda baadae kwenye vituo vya huduma hizi na kujipatia huduma kwa ufasaha zaidi”

kwa upande wake Dokta Latha Sujit wa Elite Dental Clinic alitoa wito kwa watanzania wote kuona umuhimu na kuwa na utaratibu wa kutembelea vituo vya afya na kufanya uchunguzi wa kinywa mara kwa mara.

“Sisi Elite Dental Clinic tunatoa huduma ya kuchunguza na kutibu meno, lakini wito wangu kama daktari kwa watanzania kuhusu Afya ya Kinga ya meno msisubirie mpaka usikie maumivu au tatizo litokee, nashauri familia na jamii kwa ujumla tuwe tunatenga muda na utaratibu wakwenda kwenye vituo vya Afya popote pale kwa uchunguzi na ushauri ni muhimu sana kwa Afya zetu” alieleza Dr Latha

Gulio la Airtel mbali na kuwepo na tiba hiyo ya Kinywa toka kwa Elite Dental Clinic na huduma za uchunguzi wa macho toka kwa International Eye Centre pia lilihudhuriwa na watoa huduma nyingine za kijamii wakiwemo Seifi Group wanaotoa huduma za vifaa vya elimu, 1st House (kwa huduma za mikopo ya nyumba), Superdoll (kwa huduma za matairi pamoja vipuli vya vifaa vya moto), Club9 (huduma ya mazoezi na mazoezi tiba) GT Bank, pamoja na Asas Milk.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages