Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akimshukuru meneja wa NMB kanda ya Ziwa – Abraham Augustino baada ya kupokea madawati ya shule ya msingi Mwenge kutoka NMB. NMB Ilikabidhi madawati 60 yenye thamani ya shilingi milioni tano kwaajili ya shule ya msingi mwenge ili kupunguza uhaba wa madawati kwa shule hiyo. Msaada huo ni sehemu ya misaada mbalimbali inayotolewa na NMB ambayo kwa mwaka huu, wametenga zaidi ya shilingi bilioni moja kwaajili ya kusaidia sekta ya afya na elimu.
Katibu tawala wilaya ya Songwe – Johari Samizi (tatu kushoto) akimshukuru meneja mahusiano wa NMB kanda ya nyanda za juu – Focus Lubende baada ya kupokea msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni tano kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa vifaa hivyo kwa hospitali ya Wilaya ya Songwe Mwambani. Wengine katika picha ni watumishi katika hospitali ya Mwambani na NMB. Msaada huo ni sehemu ya misaada mbalimbali inayotolewa na NMB ambayo kwa mwaka huu, wametenga zaidi ya shilingi bilioni moja kwaajili ya kusaidia sekta ya afya na elimu.
Sehemu ya akina mama wakiwa na Meneja wa huduma za Jamii kutoka benki ya NMB – Lilian Kisamba wakiwa na furaha baada ya kushuhudia makabidhiano ya vifaa vya hospitali hususani vitanda vya kujifungulia katika kituo cha Afya cha Mgango- wilayani Musoma. Msaada huo ni sehemu ya misaada mbalimbali inayotolewa na NMB ambayo kwa mwaka huu, wametenga zaidi ya shilingi bilioni moja kwaajili ya kusaidia sekta ya afya na elimu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama (Mwenye kofia) Fadhili Nkurlu akimshukuru meneja wa NMB kanda ya kaskazini – Leon Ngowi baada ya kupokea msaada wa vifaa vya ujenzi kutoka NMB. Msaada huo unatarajiwa kumalizia ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Nyasubi iliyopo mjini Kahama. Kutoka kulia ni meneja wa tawi la NMB kahama – Richard Kirenga, Mkurugenzi wa halmashauri ya kahama Andrson Msumba pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya elimu halmashauri Benard Mahongo wakishuhudia makabidhiano. Msaada huo ni sehemu ya misaada mbalimbali inayotolewa na NMB ambayo kwa mwaka huu, wametenga zaidi ya shilingi bilioni moja kwaajili ya kusaidia sekta ya afya na elimu.
BENKI ya NMB Tanzania kupitia Kitengo cha Masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) imetoa msaada wa vifaa vya hospitali, vifaa vya ujenzi wa madarasa pamoja na madawati katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Songwe na Mara.
Katika mkoa wa Mwanza, benki ya NMB imetoa msaada wa madawati 60 kwa Shule ya Msingi Mwenge yenye thamani ya Tsh. milioni tano ili kusaidia kupunguza uhaba wa madawati katika shule hiyo.
Katika mkoa wa Shinyanga, imetoa msaada wa vifaa vya ujenzi ambavyo vitatumika kumalizia ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Nyasubi iliyopo wilayani Kahama.
Pia NMB imetoa msaada kwa mkoa wa Songwe kwa kutoa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya Tsh. milioni tano ambavyo vitatumika katika hospitali ya Wilaya ya Songwe Mwambani ,vifaa hivi vinalenga kupunguza uhaba wa vifaa uliopo katika hospitali hiyo.
Hata hivyo NMB haikuishia hapo kwani pia imetoa vifaa vya hospitali vikiwepo vitanda vya kujifungulia katika kituo cha Afya cha Mgango kilichopo wilayani Musoma, Mara.
Kwa mujibu wa Meneja wa Miradi na Uwajibikaji kwa Jamii wa Benki ya NMB, Bi. Lilian Kisamba, benki hiyo imetenga Tsh. bilioni moja kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya na elimu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)