Pages

NMB TAWI MLIMANI CITY WAKIZAWADIA KITUO CHA YATIMA

IMG_0177Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City, Seka Samuel Urio (kulia) akimkabidhi Mamamlezi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Umra, Zamda Idrissa  (kushoto) sehemu ya msaada waliotoa katika kituo hicho. Misaada iliyotolewa  ni pamoja na mchele kg 100, maharagwe kg 50, sukari kg 50, mafuta ya kula lita  20, mbuzi wawili, sabuni za kufuli na dawa za meno katoni moja moja.

IMG_0182


Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City, Seka Samuel Urio (kulia) akimkabidhi mbuzi wawili Mratibu wa Kituo cha Watoto Yatima cha Umra, James Gabone (kushoto) ikiwa ni sehemu ya msaada waliotoa kwa watoto wa kituo hicho 
IMG_0199
Picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya msaada huo.

WAFANYAKAZI
 wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City jana walikitembelea kituo cha 
watoto yatima cha UMRA kilichopo Magomeni Mikumi na kuwazawadia watoto wa kituo hicho zawadi mbalimbali ikiwemo vyakula katika mfungo wa Ramadhani na vitakavyotumika katika Siku Kuu ya Idd mara baada ya mfungo mtukufu wa Ramadhani. Akizungumza wakati akikabidhi misaada hiyo, Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City, Seka Samuel Urio alisema msaada huo ni michango ya wafanyakazi wa benki hiyo katika tawi lake, ikiwa ni utaratibu wa kawaida kurejesha fadhila kwa wateja wao.

Alisema waliamua kukitembelea kituo hicho baada ya kuguswa na shughuli za kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu zinazofanywa na kituo hicho kilichopo Magomeni, Mikumi jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa vyakula vilivyotolewa na wafanyakazi hao ni pamoja na mchele kg 100, maharagwe kg 50, sukari kg 50, mafuta ya kula lita 20, mbuzi wawili, sabuni za kufuli na dawa za meno katoni moja moja.

"...Huu ni utaratibu wa kawaida kwetu kutembelea, kujumuika na kusaidia jamii hasa wenye uitaji, leo tumewazawadia watoto hawa wa kituo cha Umra vitu mbalimbali pamoja na vyakula vya mfungo wa ramadhani na vingine katika siku kuu ya Iddi inayokaribia mara baada ya kumalizika mfungo wa Ramadhani," alisema Urio.

Kwa upande wake Mratibu wa Kituo cha Watoto Yatima cha Umra, James Gabone aliishukuru Benki ya NMB kwa kutoa msaada huo ambao utasaidia watoto wao kupata chakula sasa na baadaye kwenye Siku Kuu ya Iddi, ambapo watoto huitaji faraja zaidi.

Aliziomba taasisi na watu wengine kukumbuka kuwasaidia watoto wanaoitaji msaada hasa waliopo katika mazingira hatarishi ili kujenga uhusiano mzuri na Mungu.

"...Unajua unapomsaidia muhitaji yeyote unajenga misingi ya upendo suala ambalo linasisitizwa sana na Mungu katika dini zote, tukipendana tutasaidiana na kuendeleza mahusiano mazuri na Muumba," alisema Gabone.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)