Pages

WASHIRIKI WA WAZO LA UBUNIFU WA TEKNOLOJIA YA MAPINDUZI YA KILIMO YA ABINBEV NA TBL GROUP WAPIGWA MSASA DAR

 Baadhi ya washiriki wa shindano la wazo la ubunifu wakimsikiza Meneja wa sekta ya kilimo wa ABINBEV kanda ya Afrika Mashariki, Coetzee Theunis
 Makamu wa Rais wa kampuni ya Solutions Africa Zone Lee Dowson wapili (kushoto) akifafanua jambo juu ya mashine ya kupandia nafaka iliyobuniwa na wanachama wa Better Planters Enterprise (BPE) toka Arusha
 Baadhi ya washiriki waliowasilisha mawazo yao ya ubunifu wakiwa kwenye warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na EA Agri Innovation event kwa kushirikiana na TBL Group na ABINBEV
Baadhi ya washiriki waliowasilisha mawazo yao ya ubunifu wakiwa kwenye warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na EA Agri Innovation event kwa kushirikiana na TBL Group na ABINBEV
---
Washiriki wa wazo la ubunifu wa teknolojia ya mapinduzi ya kilimo ya ABINBEV na TBL Group wapigwa msasa Dar es Salaam

Washiriki wa wazo la ubunifu la kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo watakaotangazwa katika mkutano mkubwa wa masuala ya ubunifu,matumizi ya teknolojia na ukuzaji wa sekta ya kilimo katika ustawishaji wa jamii unaojulikana kama ,The East Africa (EA) Innovation Event, utakaofanyika jijini Dar es Salaam .

Mkutano huu umeandaliwa na kampuni ya ukuzaji ubunifu wa kiteknolojia ya Bits & Bytes kwa kushirikiana na kampuni ya ABIn Bev Africa na Tanzania Breweries Limited,na umelenga kuonyesha ubunifu unavyoweza kuleta mabadiliko endelevu kwenye jamii, mojawapo ikiwa mradi wake kwa kushirikiana na wakulima wadogowadogo unaojulikana kama Smart Barley.

Utakutanisha washiriki zaidi ya 100 kutoka sekta mbalimbali ikiwemo wataalamu wa kilimo,wabunifu,wahandisi na jamii mbalimbali za wafugaji na utajikita zaidi kujadili ya kupambana na changamoto zinazowakabili wakulima wadogowadogo nchini na mikakati ya kuwawezesha kuongeza mavuno kutokana na shughuli zao za kilimo.

Meneja wa huduma za kilimo wa IBinBev Afrika Mashariki , Coetzee Theunis , alisema katika ukanda wa Afrika Mashariki wapo maelfu ya wakulima wadogowadogo wa zao la Shahiri na mtama wanaoshirikiana na kampuni ya ABInBev katika nchi za Tanzania na Uganda kupitia kampuni zake tanzu za Tanzania Breweries Limited (TBL) na Nile Breweries Limited (NBL),ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa mvua.Kwa kuwawezesha kupata teknolojia za kisasa wataweza kuongeza mavuno zaidi na maisha yao kuwa bora zaidi.

Kwa upande wake mwanzilishi wa kampuni ya Bits&Bytes Convention,Zuweina Farah Zuweina Farah,amesema kuwa mkutano wa mwaka huu unatarajiwa kuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa kwa ushirikiano na kampuni ya ABIn Bev,utajadili changamoto za wakulima wadogo na kuzitafutia ufumbuzi lengo kubwa likiwa ni kuwakwamua.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)