Pages

Wanawake wajipumzisha Kunduchi, wasema wanastahili kupumzika

 Mwandazi wa siku ya wamama (mother’s day eve party), Magdalena Gisse akizungumza kuhusu umuhimu wa siku hiyo kwa wamama iliyofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach & Resort Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Mfanyabiashara Latifa Kabange akielezea umuhimu wa wamama kuwa na muda wa kupumzika na kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali ikiwemo ujasiriamali wakati wa siku ya wamama iliyofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach & Resort Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Mkuu wa upishi wa Hoteli ya Kunduchi Beach & Resort, mama Shilpa Suchak akizungumza kuhusiana na siku ya wamama duniani ambapo huadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Mei wakati wa usiku maalum wa siku hiyo uliofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach & Resort Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Sehemu ya wamama waliojumuika pamoja kusherehekea siku ya wamama (mother’s day eve party) iliyofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach & Resort Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki
 Baadhi ya wamama walioshiriki katika picha ya kumbukumbu wakati wa sherehe za awali kuelekea maadhimisho ya siku hiyo ya wamama (mother’s day eve party) zilizofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach & Resort Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Kikundi cha Dar es Salaam Dance International (DDI CREW) kikitoa burudani kwenye usiku maalum wa sherehe za awali kuelekea maadhimisho ya siku hiyo ya wamama (mother’s day eve party) uliofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach & Resort Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Mmoja wa wamama aliyejitambulisha kwa jina la Theo Chanda katika picha ya kumbukumbu na binti yake wakati wa usiku maalum wa sherehe za awali kuelekea maadhimisho ya siku hiyo ya wamama (mother’s day eve party) uliofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach & Resort Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Sehemu ya zawadi zilizotolewa na Jack Daniel kwa wamama waliohudhuria sherehe za awali kuelekea maadhimisho ya siku hiyo ya wamama (mother’s day eve party) zilizofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach & Resort Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
DStv walikuwepo kuhakikisha sherehe hiyo ya siku ya wamama (mother’s day eve party) inaenda vyema na kutoa huduma za ving’amuzi wakati wa sherehe hizo zilizofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach & Resort Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.


WANAWAKE wamama wanastahili kupewa nafasi na jamii kupata muda wa kupumzika na kufurahia maisha kutokana na wao kuwa wafanyakazi wa mwaka mzima.

Kauli hiyo imetolewa na mwandazi wa siku ya wamama iiliyofanyika katika hoteli ya Kunduchi Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Magdalena Gisse, mama wa mtoto mmoja, mfanyakazi wa RDF alisema kwamba aliamua kuandaa siku ya wamama kutokana na ukweli kuwa mwanamke hana muda wa kupumzika na kutuliza akili yake katika maisha yake yote.

Aidha alisema sherehe hizo pia zilitumika kuwakusanya wanawake na kuwaunga na wenzao kwa lengo la kuelezana majukumu yao ya kuhakikisha wanalea watoto.

Alisema watu wazima wote wamefikia kiwango hicho kutokana na wamama zao kujitolea maisha yote kwa ajili yao na kusema pamoja na kustahili kupumzika pia wanahitaji kuheshimiwa kutokana na wajibu wao.

Alisema katika sherehe hizo waliwaalika wamama pekee kwa kuwa walitaka wapumzike bila kufikiria katika kipindi kifupi kile kuhusu watoto wao na waume zao.

Baba anaweza kurejea nyumbani akapita baa na kupumzika lakini mwanamke hawezi anakimbilia nyumbani kwa ajili ya kuangalia watoto wao kama wamekula na pia baba akirejea naye apate nafasi yake.

Kutokana na hali hiyo mwanamke mama anakuwa bize mwaka mzima hivyo anahitaji angalau muda kidogo wa kupumzika na kukutana na wanawake wenzake kuelezana namna bora ya kuendelea na ulezi na pia kupata faragha ya kufanya mapumziko kwa kuwa ukumbi una wanawake watupu.

Katika sherehe hizo  ambazo hazikujali aina ya wamama wanaofika wawe wa kisiasa, wafanyabiashara na wanawake wa majumbani walipata nafasi pia ya kujiunga na vyombo vya fedha kama mabenki na kadhalika.

Mkuu wa upishi wa Hoteli ya Kunduchi Beach & Resort , mama Shilpa Suchak alisema amefurahishwa sana na jumuiko hilo la wamama na kusema limemfurahisha sana.

Alisema ni kweli kuwa mama yuko kazini na anahitaji kupumzika na kusema kwamba sherehe hizo zinawaletea hamasha wanawake kupumzika na kujiunga na wanawake wenzao kujifunza mambo mbalimbali.

Shilpa yupo katika hoteli hiyo kwa muda sasa na anasema kazi yake ya upishi imemwezesha kusomesha watoto wake watatu na kusema wanawake wanaweza kufanyakazi ambazo zilitawaliwa na wanaume kama yake.

Mshiriki mwingine wa sherehe hizo aliyehojiwa na blogu hii Latifa Kabange ambaye alisema yeye ni mfanyabiashara alisema sherehe hizoi zimekuwa na manufaa sana kwa wanawake kutokana na ku-connect na watu wengine.

Alisema wanawake wana shughuli nyingi na matatizo mengi ambayo yanatakiwa kusikilizwa na kusaidia kuwapokea ili kuwapa nafuu.

Alisema pamoja na changamoto za kijamii amefurahishwa kuona ushiriki wa watu wengi katika sherehe hizo ambao wanaweza kuwapa moyo na ufahamu wa namna ya kukabiliana na matatizo ya kiuchumi, jamii na walezi.

Anasema akiwa mfanyabiashara anaona matatizo mengi yakiwemo ya kodi nyingi na pia wamama kutofahamu wapi pa kupata mikopo ya kujiendeleza.

Alishukuru waandalizi na kusema elimu zaidi inatakiwa kutolewa na serikali kumwezesha mama kuwa na mizigo mwepesio wa malezi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)