Pages

HERI YA MAADHIMISHO YA MWAKA MMOJA WA SPORTPESA,BADO TUNAIKUMBUKA ZIARA YA EVERTON

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa siku ya Jumatano ya Mei 9, imetimiza mwaka mmoja tangu ilipoanza uendeshaji wa shughuli zake za kibiashara nchini.SportPesa ambayo imeanzia nchini Kenya mwaka 2014, iliingia Tanzania kwa kishindo ikiwa imejidhatiti katika kusaidia kukuza sekta ya michezo ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii.Katika kutimiza azma yake, SportPesa ilianza kwa kutoa mchango wa Shilingi Milioni 50 kusaidia maandalizi ya timu ya Serengeti Boys iliyokuwa ikijiandaa na michuano ya vijana ya AFCON iliyofanyika nchini Gabon mwaka jana.

Baada ya hapo SportPesa iliendelea kuiteka sekta ya michezo nchini kwa kuingia mkataba wa udhamini wa miaka mitano na vilabu vikongwe vya Simba na Yanga pamoja na mkataba wa mwaka mmoja na Singida United.Udhamini huo ulishuhudia vilabu vya Simba, Yanga na Singida United vikishiriki michuano mipya ya SportPesa Super Cup ambayo ilikuwa na lengo na kumpata mshindi mmoja atakayechuana na klabu ya Everton.



Kwa takribani wiki moja (kuanzia Juni 5-11), uwanja wa Uhuru ulifurika mashabiki lukuki waliokuja kushuhudia ladha ya michuano hiyo ambayo pia vilabu vya Gor Mahia, AFC Leopards, Tusker na Nakuru All Stars kutoka Kenya sambamba na Jang’ómbe kutoka Zanzibar vikitoana jasho kuzisaka zaidi ya Shilingi Milioni 60.


Ziara ya Everton

Sote ni mashahidi jinsi SportPesa ilivyojitoa mhanga kuileta nchini klabu ya Everton ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu ya EPL kutembelea Tanzania na hivyo kuitangaza vyema nchi yetu kimataifa.Sahau kuhusu mashabiki waliofurika uwanja wa Taifa Julai 13 kumshuhudia Wayne Rooney akivaa uzi wa Everton kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004, dhidi ya Gor Mahia, lakini sote ni mshahidi jinsi ziara ile ilivyoleta manufaa makubwa.

Tunakumbuka jinsi sekta ya utalii ilivyonufaika ambapo Balozi wa Everton, Leon Osman alipata fursa ya kutembelea Kreta maarufu ya Ngorongoro bila kusahau jinsi uwanja wetu wa taifa ulivyoweza kurekebishwa kwenye sehemu ya kuchezea na vyumba vya kubadilishia nguo ili kufikia viwango vya kimataifa kwa Everton kuweza kuutumia.Lakini pia hatuwezei kuzisahau semina za uongozi wa Soka zilizotolewa na wataalam wa Everton kwa viongozi wetu wa soka bila kusahau kliniki za soka za vijana na misaada mbalimbali ya kijamii waliyotoa kwa wale wenye uhitaji.


Bajaji 120

Achilia mbali sekta ya michezo, lakini SportPesa pia imefanya promosheni za aina yake zilizokuwa na lengo ka kuinua kipato cha mtanzania mmoja mmoja.Shinda na SportPesa” ilikuwa gumzo kwa zaidi ya siku 170 kuanzia Oktoba mwaka jana ambapo watanzania 120 waliweza kujishindia bajaji mpya aina ya TVS KING kila siku, kila wiki.Ama hakika familia 120 zina neno la shukrani kwa SportPesa kutokana na uwezeshaji ule ambao tumeshuhudia jinsi ulivyotoa ajira kwa vijana wa kitanzania.



Sio rahisi kuilezea SportPesa kwa Makala moja kwani mambo ambayo wamefanya kwa kipindi cha mwaka mmoja ni mengi na makubwa.Kwa niaba ya wapenda michezo wote nchini, tunapenda kuitakia kampuni ya SportPesa Heri ya maadhimisho ya mwaka mmoja na hakika hatutaweza kuisahau ziara ya Everton kwani ilimfumbua macho kila mmoja wetu na kuona kuwa kila jambo linawezekana kama tukiweka nia.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)