Pages

WAANDISHI WA HABARI WAMEFANYA KAZI KUBWA MKOANI RUVUMA.

NA DITHA NYONI.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma CHRISTINA MNDEME amewaponeza waandishi wa habari wa mkoa wa RUVUMA kwa mshikamano wao katika kazi wanazozifanya katika mkoa huu.
Kauli hiyo imeitolewa na mkuu wa wilaya ya SONGEA POLOLET MGEMA wakati akimwakilisha mkuuu wa mkoa wa Ruvuma CHRISTINA MNDEME katika siku ya uhuru wa vyombo vya habari.
Pongezi hizo zinatokana na jitihada za kuutangaza mkoa wa Ruvuma katika Nyanja zote za kiuchumi,kitamadauni ,kisiasa,kidini na kijamii ,kwani kila habari inayorushwa katika vyombo vya habari hapa nchi lazima utakutana na habari inayotoka mkoa wa RUVUMA.

Aidha MGEMA amesema waandishi wahabari wanawajibu mkubwa katika kuhakikisha wanakosoa pale wanapoona mambo hayaendi sawia ili mamlaka husika iweze kuchukuliwa na kutafutiwa ufumbuzi,
mdau mbalimbali wa habari watafurahi kwani kufanya hivyo itasaidia sana katika kuufanya mkoa kuwa mbele katika maendeleo.
“nyinyi waandishi wa habari mmetumia kalamu yenu kwa maadili mazuri katika mkoa huu wa RUVUMA.“

Hivyo kila mwandishi wa habari anawajibu wa kulinda taalamu kwa kuzingataia maadili ya kazi yake.

Aidha kuhusu kuepukana na wandishi wasio na sifa maarufu kama MAKAJANJA ,mkuu wa wilaya amesema waandishi wanawajibu wa kuliangalia kwa jicho la mbele kwa wale wanaopotosha UMMA kwa kujiita wao wandishi kumbe hawana sifa hizo,na hawapaswi kuvumiliwa hata mara moja

Kila ifikapo mei 5 ya kila mwaka duniani kote huadhimishwa siku ya uhuru wa vyombo vya habari, hapa Tanzania kitaifa imeadhimishwa katika jiji la Dodoma,na kila mkoa wa wameadhimishwa pia .


 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)