BENKI ya NMB kupitia sera yake ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) imetoa msaada katika hospitali na shule zilizopo wilayani Musoma na Musoma Vijijini wenye thamani ya Sh. 15 milioni.
Akizungumza kuhusu msaada huo, Meneja wa Kitengo cha Uwabikaji kwa Jamii (CSR) cha benki ya NMB, Lilian Kisamba amesema msaada huo unalenga kusaidia kupunguza changamoto zinazoikabili sekta ya afya na elimu.
“Tumekabidhi madawati 50 katika Shule ya Msingi Mwisenge, ni shule ambayo alisoma Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, madawati yenye thamani ya Sh. 5 milioni, “Lakini pia tumetoa msaada Musoma Vijijini ambapo tumekabidhi vitanda vya kujifungulia na vitanda vya kulalia wagonjwa, jumla ya vitanda nane pamoja na mashine za Shinikizo la Damu (BP) katika Kituo cha Afya cha Mugango zenye thamani ya Sh. 5 milioni,” alisema Kisamba.
“Pamoja na hayo tumetembelea Shule ya Msingi Kwibara kuangalia jengo ambalo tumetoa msaada wa vifaa vya kuezeka ambalo tayari tumekutaka limeshaezekwa. Tulitoa vifaa vya Sh. 5 milioni.”
Aidha, Kisamba alisema katika ziara hiyo walitembelea hospitali na shule ambazo walizipatia msaada miaka kadhaa iliyopita ambapo wameridhishwa na matumizi msaada waliotoa kwamba ulitumika kama walivyopanga utumike.
Alisema wametembelea Hospitali ya Nyasho na Shule ya Msingi Kwibara, Shule ya Msingi Busumi, Shule ya Msingi Bwai, Shule ya
Msingi Chanyauru, Shule ya Msingi Kiriba na Shule ya Sekondari Kiriba na zote zipo wilaya ya Musoma Vijijini.
“Mara nyingi tukitoa msaada huwa tunakaa baada ya muda alafu tunawatembelea ili kuweza kufanya tathmini na ufuatiliaji wa
maendeleo ya msaada tuliotoa. Hao tuliwapa msaada kati ya mwaka 2015 na 2016 ambapo mpaka sasa tumebaini vifaa tulivyotoa bado vipo katika hali nzuri na hii inatupa hamasa ya kuendelea kusaidiana na serikali kusaidia maendeleo ya jamii.
“Lakini pia walimu na wanafunzi waliongea kuhusu msaada tuliowapatia kuwa umewasaidia sana ingawa wamesema bado kuna changamoto kwani ongezeko la wanafunzi bado lipo ila madawati ni yaleyale hivyo wanaomba wadau wawasaidie.” Banki ya NMB PLC
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)