NMB kuwalipia Madeni Wadaiwa wa bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

NMB kuwalipia Madeni Wadaiwa wa bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na wanahabari kuelezea punguzo kubwa la riba kwa mikopo ya waajiliwa binafsi na wale wa Serikali. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Phidelis Joseph na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Wateja wadogo na wa kati kutoka Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Phidelis Joseph (wa tatu kulia) wakiwaongoza meza kuu zoezi la kushikana mikono pamoja kuonesha umoja kwenye hafla ya NMB kutoa punguzo kubwa la riba kwa mikopo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Phidelis Joseph (katikati) akizungumza kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Bi. Ineke Bussemaker na Sara Fihavango wa Bodi ya mikopo.
Sehemu ya washiriki katika hafla hiyo.

BENKI ya NMB imepunguza kiwango cha riba katika mikopo yake kwa wateja kutoka asilimia 19 hadi 17 kwa wateja wanaokopa kupitia mishahara kwa waajiriwa wa mashirika ya umma na wale wa binafsi.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker alisema benki hiyo imechukua hatua hiyo ikiwa ni utaratibu kupunguza riba kwa wateja wake.

Alisema punguzo hilo limegusa viwango vyote vya mikopo kwa kutumia mishahara kutoka kiwango cha chini cha shilingi 200,000 hadi cha juu cha shilingi milioni 150 kutegemea mshahara wa mkopaji.

Aliongeza kuwa ili kujenga mazingira mazuri kwa wateja wao mikopo yao sasa inashughulikiwa ndani ya saa 24 hadi muhusika anapokea mkopo wake.


 “…Wateja wetu wengi wa mikopo wamekuwa wakiomba tupunguze riba za mikopo yetu jambo ambalo tumelizingatia kwa sasa…na tumeongeza ofa ya gharama bure za kushughulikia mikopo hiyo kwa wiki sita kuanzia leo,” alisema Bi. Bussemaker.


Aliongeza NMB inasikiliza zaidi ushauri wa wateja wake na ndio maana sasa wameongeza muda wa marejesho ya mikopo kutoka kiwango cha chini cha miezi 60 hadi miezi 72 (sawa na miaka mitano hadi sita).

Ongezeko hilo la muda wa kulipa marejesho linaweza kuwanufaisha pia wadaiwa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), ambapo mkopaji anaweza kuzungumza na benki kisha ikalipa mkopo wote naye akaendelea kulipa taratibu kwa mujibu wa makubaliano na benki hiyo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages