Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Microfinance Association (TAMFI), Joel Mwakitalu (kulia) akikabidhi cheti kwa mshindi wa tatu wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Lydia Majoro wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mjasiriamali mlemavu aliyefanya vyema Aneth Geraw ambaye aliondoka na kitita cha dola za Marekani 2000 wakati hafla ya kukabidhi tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) akikabidhi cheti kwa mshindi wa pili wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Anney Sekulasa (kushoto) katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo katikati ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila.
Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) na Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (katikati) kwa pamoja wakikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Yetu Microfinance, Attemius Millinga (kushoto) ambapo taasisi yake imekuwa na ubunifu mkubwa wa bidhaa zake sambamba na mifumo ya kutolea huduma na methodolojia wakati wa hafla fupi ya tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanamke aliyefanya vyema kwenye ujasiriamali mdogo, Lucy Kiongosi akipozi baada ya kupokea cheti kilichoambatana na dola za Marekani 2000 wakati wa hafla ya tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika mwishoni wa wiki jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso.
Mshindi wa tatu wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Lydia Majoro akifurahi na kupozi na cheti pamoja na tuzo yake.
Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (katikati) akikabidhi cheti kwa Mjasiriamali mdogo aliyefanya vyema mwenye umri wa miaka 18-25 tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Mopaya Madi (kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia).
Mshindi wa jumla wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Beula Seed and Co & Sons, Zabron Mbwaga (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Microfinance Association (TAMFI), Joel Mwakitalu (wa pili kushoto), Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) akikabidhi cheti kwa Ofisa mikopo Rose Chacha (kushoto) wakati wa hafla fupi za tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila.
Na Mwandishi Wetu
Zabron Mbwaga ambaye ni Mzalishaji mbegu, aliyepo Viwanja vya NaneNane, Njiro mkoani Arusha ametwaa tuzo ya mshindi wa jumla wa tuzo za Ujasiriamali ya Citi Foundation. Tuzo hiyo inaambatana na fedha taslimu dola za Marekani 7,500.
Mbwaga ambaye aliwezeshwa upanuzi wa shughuli zake kwa mikopo kutoka BRAC Tanzania, alianza kazi zake akiwa na mtaji wa shilingi milioni 2 kabla ya kuongezewa nguvu na BRAC.
Tuzo hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki zilitolewa kwa wajasiriamali 16 na ofisa mikopo mmoja.
Mshindi wa pili ni Anney Sekulasa akiondoka na dola za Marekani 6000 huku mshindi wa tatu ni Lydia Majoro ambaye aliondoka na dola za Marekani 4000. Nafasi ya mjasiriamali mlemavu ilitwaliwa na Aneth Geraw aliyepata dola za Marekani 2000.
Zaidi ya shilingi milioni 70 za kitanzania zimetolewa kwa washindi wa kwanza hadi wa 16 . Pia Taasisi za kifedha za wajasiriamali wadogo na wa kati (MFI) zenye ubunifu mkubwa wa bidhaa zake na huduma, mifumo ya kutolea huduma na methodolojia pia ilipata tuzo. Safari hii Yetu Microfinance ndio walioinyakua.
Tuzo hizo za Citi Bank Foundation zimeendeshwa na Mtandao wa Asasi zinazotoa huduma za kifedha kwa wajasiriamali wadogo (TAMFI) ‘TAMFI’ na washindi wametangazwa na majaji walioshiriki kufanyakazi hiyo.
Tuzo hizo zimelenga kuhamasisha wajasiriamali kutumia taasisi za kifedha za watu wa kati na chini na kufaidika nazo.
Takribani wajasiriamali 209 waliwasilisha miradi yao lakini 22 pekee ndio waliweza kupenya na 16 ndio walipata ushindi wa tuzo tofauti.
Safari hii washiriki walitoka maeneo mbalimbali nje ya Dar es Salaam tofauti na ilivyokuwa kwa mwaka 2016 ambapo washiriki wake walikuwa ni wa Dar es Salaam pekee.
Washindi wengine ni Comelord Swai $ 1000, Prisca Kayombo $ 1000, Rahim Kalyango $ 1000, Emmanuel Lazaro $ 1000, Jumanne Findisha $ 1000, Salma Said $ 1000, Editha Lukindo $ 1000, Amon Kalumuna $ 1000, Salum Chumu $ 1000 na Doroth Sambi $ 1000.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)