MAASKOFU,WACHUNGUJI KANDA YA ZIWA WABARIKI TAMASHA LA PASAKA 2018,WAMPONGEZA MSAMA PROMOTIONS. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MAASKOFU,WACHUNGUJI KANDA YA ZIWA WABARIKI TAMASHA LA PASAKA 2018,WAMPONGEZA MSAMA PROMOTIONS.


MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo mbele ya Maaskofu na Wachungaji wa mkoa wa jiji la Mwanza mapema leo jijini humo kuhusu upokeo na maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika hapo kesho Aprili Mosi,ndani ya  uwanja wa CCM Kirumba mkoani humo.
MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na Maaskofu na Wachungaji wa mkoa wa jiji la Mwanza mapema leo kwenye moja ya hoteli jijini humo,akieleza kukamilika  rasmi kwa maandalizi ya tamasha la pasaka,linalotarajiwa kufanyika hapo kesho Aprili Mosi katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani humo.

Msama amewashukuru Maaskofu hao na Wachungaji kwa kujitoa na kuunga mkono Tamasha la Pasaka 2018,ambalo kwa mara ya kwanza linaanzia kufanyika jijini Mwanza na baadae kuhamia mkoa wa Simiyu ndani ya mji wa Bariadi April 2 ndani ya uwanja wa Halmashauri,aidha tamasha hilo litakuwa na waimbaji lukuki ambao tayari wameishatangazwa kushiriki,kuhakikisha tamasha hilo linafana.
 
Kwa upande wa Maaskofu wameipongeza Kampuni ya Msama Promotions,chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama kwa kuupa mkoa wa Mwanza kipaumbele kwa kuleta tamasha hilo mkoani humo,Wameongeza kuwa tamasha hilo litawavuta waumini wengi na wapenzi wa muziki wa injili na kuwaleta pamoja ili kupata neno la mungu na uponyaji kwa njia ya uinjilisti wa nyimbo za injili .
katika picha kutoka kushoto ni Askofu Charles Sekelwa Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Mwanza na Askofu Zenobius Isaya kutoka kanisa la Philadephia Gospel Asembly na mlezi wa Msama Promotion Kanda ya Ziwa.

Askofu
Zenobius Isaya kutoka kanisa la Philadephia Gospel Asembly na mlezi wa
kampuni ya Msama Promotion Kanda ya Ziwa,akitoa ufafanuzi wa namna
tamasha hilo la Pasaka 2018 lilipofikia na maandalizi yake kwa
ujumla,mbele ya kikao cha Maaskofu na Wachungaji kilichofanyika mapema
leo jijini humo,kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama na
kushoto ni Askofu Charles Sekelwa Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa
Mwanza.

Mmoja wa maaskofu akitoa mchango wake katika kikao hicho kilichofanyika jijini Mwanza leo.
Askofu Joyce Mangu wa kanisa la Calvary Assemblies Of God Mjini Kati jijini Mwanza akizungumza wakati akitoa mchango wake katika kuboresha tamasha hilo siku za usoni na kwamba amefurahishwa sana na ujio wa tamasha hilo kwa jiji la Mwanza.




Baadhi ya maaskofu na wachungaji wakifuatilia kikao hicho. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages