Pages

Itikadi za kisiasa Dar zinarudisha nyuma maendeleo - Madiwani

 
Diwani wa Kata ya Kivule, Wilson Molel (kulia) akizungumza kwenye semina iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa madiwani wa Mkoa wa Dar es Salaam kuangalia namna wanavyoweza kuandaa bajeti zitakazo tatua moja kwa moja changamoto za wananchi 
Diwani Viti Maalum Kata ya Saranga, Ubungo, Liberata Samsoni (kulia) akichangia mada kwenye semina iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa madiwani wa Mkoa wa Dar es Salaam kuangalia namna wanavyoweza kuandaa bajeti zitakazo tatua moja kwa moja changamoto za wananchi. 
Diwani wa Kata ya Kipunguni, Ukonga, Mohamed Msophe akichangia mada katika kikao hicho. 
Afisa Programu, Uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deogratius Temba (kushoto) akiwasilisha mada kwenye semina iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa madiwani wa Mkoa wa Dar es Salaam kuangalia namna wanavyoweza kuandaa bajeti zitakazo tatua moja kwa moja changamoto za wananchi.

VITENDO vya kuingiza itikadi za kisiasa vinavyofanywa na baadhi ya madiwani wa vyama mbalimbali jijini Dar es Salaam vinaendelea kukwamisha juhudi za maendeleo na huduma za kijamii kwa wananchi maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam. Kauli hiyo imetolewa jana na baadhi ya madiwani wa Mkoa wa Dar es Salaam walipokuwa wakijadiliana katika semina iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa madiwani hao kuangalia namna wanavyoweza kuandaa bajeti zitakazo tatua moja kwa moja changamoto za wananchi wao.

Diwani wa Viti Maalum, Halmashauri ya Ubungo, Rehema Mayunga itikadi za kisiasa zinazoendekezwa na baadhi ya madiwani wa Dar es Salaam kwa baadhi ya maeneo zinakwamisha juhudi za maendeleo kwa wananchi, huku akiwataka madiwani kushirikiana na kuondoa itikadi hizo ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Alisema linapokuja suala la kuwaletea maendeleo wananchi kila diwani bila kujali chama chako au itikadi niwajibu wa wanasiasa hao kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha jamii wanaoiwakilisha inapata maendeleo. "...Binafsi mimi nimezunguka na kutoa elimu kwa akinamama na wananchi wengine kuungana katika kuleta maendeleo kwenye maeneo yao, tuache kuingiza siasa kila jambo Serikali ya sasa haitaki kuendekeza siasa tufanye kazi," alisema Diwani huyo wa Viti Maalum.

Akizungumza Diwani wa Kata ya Kivule, Wilson Molel alisema suala la kuingiza siasa katika kila jambo la maendeleo zikiwemo hata huduma za kijamii limekuwa likichelewesha na hata kukwamisha maendeleo ya wananchi hivyo kuwataka madiwani kuwaachia wataalam wafanye kazi na kuacha kuingiza itikadi za kisiasa kwa kila jambo. "...Ifike mahali wanasiasa tuwaache wataalam wetu wafanye kazi pale wanapoitajika tuache kufanya siasa kwa kila jambo...," alisema Molel.

Aidha Diwani wa Kata ya Zingiziwa, Hussein Togoro alisema madiwani ni wasimamizi wa demokrasia katika maeneo yao hivyo kushauri uwepo wa siasa safi zisizo na ubaguzi kwa vyama jambo ambalo linaweza kumaliza changamoto za baadhi ya maeneo.

Sisi ni wasimamizi wa demokrasia katika maeneo yetu...hivyo tujitahidi kufanya siasa safi zisizo na ubaguzi hasa katika masuala ya maendeleo na huduma za kijamii. Tukifanya hayo tutaweza kuchochea maendeleo kwa jamii," alisisitiza diwani huyo.

Kwa upande wake, Afisa Programu, Uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deogratius Temba awali akiwasilisha mada aliwaomba madiwani hao kuhakikisha mikutano ya kisheria iliyoainishwa kwenye sheria namba 7/1982 ya mamlaka za wilaya na 8/1982 ya mamlaka za miji inafanyika kwa wakati na kuweka kwenye ubao wa matangazo maazimio ya serikali za vijiji/Mitaa na mapato na matumizi ya fedha za umma.

Aliwashauri kutenga asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri kuwezesha vijana asilimia 4, wanawake asilimia 4 na watu wenye ulemavu asilimia 2 na kufuatilia utekelezaji wake. Kutenga fedha kwaajili ya kukarabati na kujenga miundombuni muhimu ya kiuchumi na kijamii katika sekta zote kama afya, madarasa, nyumba za walimu, mabweni, maabara, matundu ya vyoo shuleni, na kumalizia miradi iliyokwama iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi.

"Tujitahidi kuweka wazi hesabu za mapato na matumizi ya serikali za Mitaa/ Kata, kuitisha mikutano ya kisheria na kutoa mirejesho ya shughuli za maendeleo," alisema Temba.

[caption id="attachment_84190" align="aligncenter" width="500"] Sehemu ya washiriki wa kwenye semina iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa madiwani na watendaji wa Serikali wa Mkoa wa Dar es Salaam kuangalia namna wanavyoweza kuandaa bajeti zitakazo tatua moja kwa moja changamoto za wananchi.[/caption]



[caption id="attachment_84192" align="aligncenter" width="500"] Baadhi ya washiriki kwenye semina hiyo wakichangia mada anuai.[/caption]



[caption id="attachment_84209" align="aligncenter" width="500"] Mkutano huo ukiendelea[/caption]

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)