Pages

'YATOSHA MITANDAO YOTE' YAJA KWA UHURU WA MAWASILIANO

 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari baada ya uzinduzi bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Beatrice Singano na kushoto Afisa Mkuu wa Biashara Rohit Tandon
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Sunil Colaso, Mkurugenzi wa Mawasiliano Beatrice Singano na kushoto Afisa Mkuu wa Biashara Rohit Tandon, wakionyesha bango baada ya kuzindua bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari baada ya uzinduzi bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Sunil Colaso

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza uhuru wa mawasiliano kwa kuzindua huduma kabambe ya kipekee kwa wateja wake wanaopiga simu na kutuma sms kwenda mitandao yote nchini. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzindua wa Yatosha Mitandao Yote, Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema kuwa “wateja wanabaki kuwa ndio nguzo kuu yetu kwenye biashara, ni furaha kubwa kwetu kuzindua huduma ya Yatosha Mitandao Yote ambayo itawapa wateja wa Airtel unafuu zaidi na uhuru wa kutumia huduma za mawasiliano. Tunaendelea kufanya utafiti kufahamu mahitaji ya wateja pamoja na kuongeza ubunifu ili kuleta huduma nafuu zaidi ”

“Tunaipongeza serikali yetu kwa kupunguza gharama za kuunganisha simu mitandao mingine kutoka Shilingi 26.96 kwa dakika hadi shilingi 15.6 kwa dakika kuanzia januari, Airtel tunaona fahari sana kuwapa wateja wetu unafuu huo kupitia huduma yetu ya Yatosha Mitandao Yote. Mteja anatakiwa kuwa tu na laini iliyosajiliwa ya Airtel ili kufurahia huduma zetu bora na nafuu” aliezeza Colaso

Yatosha Mitandao Yote inawafanya wateja kufurahi na kufanya mipango ambayo inayoendana na hali ya maisha na kutoa Uhuru wa kuunganisha familia, marafiki na wanafanya biashara kupitia mtandao wa Airtel kwenye mitandao mingine nchini kote na kwa muda wowote.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kuwa “Airtel tumeboresha upya huduma ya Yatosha bando ili kuongeza muda wa mangezi na kupanua uhuru kwa kutoa fursa kwa wateja kutumia huduma ya Yatosha Mitando Yote kwa kutuma sms, kupinga simu kwenda mitandao yote kwa kuanzia shilingi 600 tu. Ukiwa na Airtel Yatosha mahitaji yako ya mawasiliano yametimia!

“Kwa kujiunga na Yatosha Mitando Yote, wateja watatakiwa kupinga *149*99# halafu changua 3 ili kununua bando ya ‘Yatosha Mitandao Yote’ kulingana na mahitaji yako. Tuna uhakika kuwa huduma ya Yatosha Mitandao Yote itarahisisha maisha” alisisitiza Bi Singano

Yatosha Mitandao Yote ni moja ya bidhaa za Airtel Yatosha, Airtel hivi karibuni pia ilizindua bando za intaneti za Yatosha SMATIKA Intaneti ambayo inatoa 2GB kwa Tzs 2000 ambazo zinadumu kwa siku 3. Wateja wa Airtel wanaojiunga na Smatika bando wanajishindia simu mpya za smartphone, modem na 1GB kwa wateja 1000 kila siku.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)