Pages

MWIMBAJI MARTHA BARAKA KUNOGESHA TAMASHA LA PASAKA 2018 NDANI YA KANDA YA ZIWA

Mmoja wa waratibu wa tamasha la Pasaka 2018, RainFred Masako (kati) akizungumzia maandalizi ya tamasha la Pasaka 2018 yanayotarajia kufanyika Kanda ya Ziwa katika mikoa ya Mwanza na Simiyu. Pembeni ni Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Martha Baraka na Meneja wa Msama Promotions Ltd, Jimmy Charles mapema leo jijini Dar es Salaam.

Masako amesema kuwa wakati umefika kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kujipatia  burudani ya muziki wa njili kutoka kwa waimbaji mbali mbali ambao mpaka  sasa wamethibitisha kushiriki kwao.
 Mmoja wa waimbaji mahiri wa nyimbo za injili Martha Baraka akieleza namna  alivyojiandaa katika tamasha la pasaka 2018,mapema leo mbele ya  Waandishi wa habari (hawapo pichani). Kushoto ni Meneja wa Msama Promotions Ltd, Jimmy Charles.

Maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2018 yameendelea kunoga huku waimbaji mbali mbali wakiendelea kutambulishwa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, RainFred Masako wakati akimtambulisha mwimbaji wa nyimbo za injili Martha Baraka.

Masako amesema kuwa wakati umefika kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kujipatia burudani ya muziki wa njili kutoka kwa waimbaji mbali mbali ambao mpaka sasa wamethibitisha kushiriki kwao.

Kwa upande wake mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Martha Baraka amesema kuwa yupo tayari kuwapa burudani wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake kwa vile amejiandaa vyema."Tunaomba wakazi wa Kanda ya Ziwa mjitokeze kwa wingi kuhudhuria Tamasha hilo ambalo nitaungana na waimbaji wenzangu kutoa burudani ya kukata na shoka," amesema Martha Baraka.

Tamasha hili linatarajiwa kufanyika Aprili 1-2, 2018 kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Uwanja wa Halmashauri mkoani Simiyu,ambapo Mwimbaji nyota wa nyimbo za Injili Rose Muhando atazindua albamu yake mpya.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)