Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Edicome Shirima akizungumza kufungua mkutano wa wadau wa elimu ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kusaidia maboresho ya elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Tixon Tuyangine Nzunda akizungumza katika mkutano wa wadau washiriki kwenye mradi wa kuboresha elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam. Mtafiti Mwandamizi na Kiongozi wa Kitengo cha Elimu na Uwezeshaji Vijana wa African Population and Health Research Center (APHRC) Moses Ngware akizungumza katika mkutano kwa wadau wa elimu ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kusaidia maboresho ya elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam. Meneja Programu wa Mtandao wa Elimu Tanzania, (TenMet), Bw. Nicodemus Shauri Eatlawe (kushoto) akiwasilisha mada katika mkutano huo. Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akichangia mada katika mkutano wa wadau washiriki kwenye mradi wa kuboresha elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam. Mmoja wa washiriki katika mkutano wa wadau washiriki kwenye mradi huo akichangia mada. Mkutano huo ukiendelea.
BAADHI ya watendaji wa Serikali, Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) na taasisi ya African Population and Health Research Center (APHRC) wamekutana na kufanya majadiliano ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam.
Akizungumza katika kikao na wadau hao waliokutana leo mjini Dodoma, Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Edicome Shirima alisema Serikali imeliona tatizo la msongamano wa watoto mtaani na ndio sababu ya kuja na utaratibu wa elimu bila ada.
Alisema utaratibu wa elimu bila malipo haumnyimi mzazi kuendelea kumwezesha mtoto wake kupata chakula awapo shuleni, hivyo kama wazazi watakubaliana kuwawezesha wanafunzi wao kupata chakula kwa utaratibu mzuri wanaweza kufanya hivyo bila vikwazo kutoka serikalini.
"...Haijazuiliwa mzazi kumlisha mtoto wake shuleni, wazazi kuweka utaratibu mzuri wa kuwalisha watoto wao wanapokuwa shuleni kwa makubaliano haijazuiliwa...tusaidiane kuelimisha umma kwa hili," alisema Dk. Edicome Shirima.
Alisema mbali na Serikali kuondoa ada shuleni bado kuna wazazi hawapeleki watoto shule, hivyo kuwaomba wabunge kuanza mchakato wa kuja na sheria itakayowabana wazazi wa aina hiyo.
Kwa upande wake Meneja Programu wa Mtandao wa Elimu Tanzania, (TenMet), Bw. Nicodemus Shauri Eatlawe akiwasilisha mada kwa wajumbe hao aliwataka kushirikishana mawazo ili baadaye kutoka na mapendekezo yatakayoboresha zaidi utekelezaji wa mradi huo wa kuboresha elimu kwa makazi yenye msongamano.
Alisema utafiti wa awali walioufanya kwa baadhi ya shule za maeneo ya mradi unaonesha kumekuwa na changamoto nyingi kwa wanafunzi kutokana na msongamano uliopo mashuleni jambo ambalo linahatarisha usalama kiafya kwa wanafunzi na hata kitaaluma katika masomo yao.
changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto na elimu inayotolewa katika maeneo ya miji yenye msongamano kwa kuanzia na Jiji la Dar es Salaam, mradi huo pia unaweza kuendelezwa katika miji ya mikoa mingine hapo baadaye.
Mradi huo utakao saidia maboresho ya elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam utakao tekelezwa kwa miaka miwili na unaweza kusabazwa katika maeneo mengine ya Tanzania yenye changamoto hizo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)