Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe (kulia) akimkabidhi tuzo ya ushindi wa Mamlaka inayotoa huduma bora za Maji Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA) ,Prof. Faustine Bee. Kushoto ni Mkurugenzi Mkurugenzi Mkuu wa MUWSA, Joyce Msiru. Makabidhiano hayo yalifanyika mjini Dodoma juzi.
******************
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji,Aisack Kamwelwe ameiagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) kuukagua mradi wa maji wa Buchosa uliopo Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza kwani anazotaarifa kuna vifaa vimenunuliwa havina ubora kabisa.
Maagizo hayo aliyatoa jana Mjini hapa wakati akizindua ripoti na utendaji wa Mamlaka za Maji za Miji na Mikoa na miradi ya kitaifa.
Uzinduzi huo uliandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ambapo Mamlaka ya Maji ya Moshi ilichaguliwa kuwa ya kwanza kwa utoaji bora wa huduma za maji.
Waziri Kamwelwe alisema alienda kuungalia mradi wa Buchosa na kutoridhishwa nao kutokana na mabomba yaliyonunuliwa kutokuwa na ubora hivyo ameiagiza Takukuru wakaungalie ili kujua ubadhilifu uliofanyika.
“Bosi wa Takukuru upo hapa siwezi kukuagiza lakini kuna huu mradi wa maji wa Buchosa mabomba yaliyonunuliwa ni ya Class B wakati mabomba hayo yanatumika sehemu ambayo maji hayana ‘Pressure’ pamoja na kwenye majitaka,”alisema Kamwelwe.
Aidha Waziri Kamwelwe ameziagiza Mamlaka za Maji kutafuta maeneo kwa ajili ya kutupa maji taka ili kupunguza magonjwa ya milipuko kama Kipindupindu.
“Hasa kwenye Mji Mkuu kama hapa Dodoma ni lazima tutenge maeneo kwa ajili ya maji taka,”alisema Kamwelwe.
Katika hatua nyingine, Waziri Kamwelwe ametoa mwaka mmoja kwa Mamlaka za Maji za Lindi,Mpanda,Bariadi na Geita kujitathmini na kubadilika kwani haridhishwi na utendaji kazi wao.
‘Niwashauri msitukimbie wazee kwenye maamuzi yenu sio mtu anatoka Chuo miaka mitatu tu anapewa mradi lazima ataharibu kwani hana uzoefu,’alisema Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Ewura,Profesa Jamidu Katima alisema utoaji wa huduma za maji taka ni tatizo nchini kutokana na kutolewa na sekta binafsi.
‘Lazima tuweke utaratibu ukiwemo wa kutibu maji ili kuondoa tatizo la ugonjwa wa Kipindupindu,”alisema
Naye Mwenyekiti wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mjini Moshi (MUWSA) Profesa FaustiNE Bee ambao ndio washindi wa wanaotoa huduma bora za maji,alisema usafi unaopatikana katika Mji huo unasababishwa na upatikanaji wa maji.
“Kwa sasa maji upatikanaji wa maji ni kwa masaa 23.5 hapo tunakosa 0.5 ndani ya masaa 24, hivyo tumejipanga kuhakikisha hiyo 0.5 tunaiondoa na kuwa masaa yote maji yanapatikana katika Mji wa Moshi,”alisema
Naye Kaimu Mkurugenzi wa EWURA Mchami alisema uzalishaji wa maji safi kwa sasa umeongeza toka lita 248 hadi 276 kwa 2016/2017, jambo ambalo linatia moyo kutokana na hali hiyo.
Alisema kutokana na hilo hata wateja pia wameongezeka kwa sababu lita za ujazo zimeongezeka kutokana na kuwa mamlaka zinafanya kazi kwa karibu na wateja wao wa maji hapa nchini.
Hata hivyo Waziri aliwapongeza mamlaka hizo kutokana na utendaji uliashiria kwamba wanawajali wateja na kuwataka waongeze bidii zaidi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)