Pages

IGP SIRO MGENI RASMI UZINDUZI WA CHAMA CHA WAMILIKI WA MBWA

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania  Canine Association Ltd (TCAL) Sinare Sinare, akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati akitangaza uzinduzi rasmi wa Chama cha Wamiliki wa Mbwa utakaofanyika katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni tarehe 3 February ambapo Mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Inspector General wa Polisi (IGP) Simon Siro. Kushoto kwake ni Wajumbe wa Kamati ya uzinduzi huo, Felician Bulu na Deo Rweyunga. (kushoto) ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Mbwa na Farasi, Dkt. Egyne Emmanuel. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Mkutano ukiendela....
Na Amina Kasheba, Dar (DSJ)
INSIPEKTA wa polisi (IGP) Simon Siro atanatarajia kuwa
mgeni ramsi katika uzinduzi wa chama cha mbwa kilichoundwa na Tanzania Canine  Assoation limited (TCAL) wafuga mbwa wa Tanzania
Uzinduzi huo unatarajia kufanyika Febuari 3 mwaka huu na kushirikishwa na wasio kuwa wanachama ili kuleta ushirikiano katika masuala ya wafugaji Tanzania.

Akizungumza na mwandishi  wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Dar es salaam leo,  Mkurungenzi   wa kampuni ya Tanzania Acanine Association Limited (TCAL) Dk. Sinare Sinare,  alisema dhumuni ya kuanzisha chama hicho ni kuwakutanisha wadau mbalimbali na wamiliki wa mbwa Tanzania ili kujenga ushirikiano baina ya wanachama wenyewe kwa lengo la kusimamia na kushauri kuhusu uzalishaji mbwa bora.

Aidha alisema wameamua kuanza kuhamasisha ufugaji bora wa mbwa ikiwa ni pamoja na kushawishi ufugaji unaojali maslahi na faida  ya wanyama mbwa katika jamii na kutoa ushauri wa jinsi ya kusimamia ili kupata zao bora la Mbwa.  “Dhumuni la kuanzisha chama hicho ni kuwakutanisha wadau na wamiliki wa mbwa Tanzania, ili waweze kuwa na sauti ya pamoja
kama wamiliki wa Mbwa Tanzania,

Aliongeza kuwa katika uzinduzi huo hakutakuwa na kiingilio ambapo mtu yoyote anaruhusiwa kuhudhuria na kujionea michezo mbalimbali ya Mbwa na Farasi. Katika kusherehesha uzinduzi huo pia kutakuwa na maonyesho mbalimbali kutoka Kikosi cha mbwa ambao wataonyesha uwezo wa mbwa wao katika kulinda uslama wa raia na mali zao, pamoja na michezo ya farasi.

Baada ya uzinduzi huo itakuwa ni sehemu ya maandalizi ya maonyesho makubwa ya mbwa yanayotarajia kufanyika Juni 6 mwaka huu  na kushirikisha washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika.   

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)