Pages

Uzinduzi wa Tanzania Canine Association Kufanyika tarehe 3 February Leaders Kinondoni DSM

Mnamo Tarehe 3 February 2018 Kwa mara ya kwanza Tanzania inaingia katika Historia ya Kusajili Chama cha Wapenzi wa Mbwa kikijulikana kama Tanzania Canine Association ambapo Kwa mara ya kwanza chama hiki kinazinduliwa katika Viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni

Uzinduzi huu utaanza saa nne asubuhi mpaka majira ya saa kumi na mbili jioni  pia Kutakuwepo na Maonyesho ya Mbwa katika shughuli mbalimbali Kama vile Utii, Kushambulia, Kung'ata na Kuzuia ambapo pia wapenzi na wadau wa mbwa wataweza kupata nafasi ya kujifunza maswala mbalimbali ya Kitaalamu katika Ufugaji mzuri na wa kisasa wa Mbwa wa aina zote lakini pia wataweza kupata nafasi mbalimbali za kukutana na kuonana ana kwa ana na wazalishaji mbalimbali wa aina mbalimbali za mbwa wa Hapa Tanzania.

Katika Uzinduzi huo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Polisi Tanzania Mh IGP Simon Sirro 

Karibu sana ili kuweza kufahamu aina mbalimbali za Mbwa na Kujifunza ufugaji bora wa iana zote za mbwa nchini kwa Maendeleo na Ustawi wa Mbwa Tanzania

Hakuna kiingilio na nyote mnakaribishwa

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)