BINSLUM ATAKA MSHIKAMANO COASTAL UNION - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

demo-image

BINSLUM ATAKA MSHIKAMANO COASTAL UNION





IMG_2313
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza katika hafla ya
kuwapongeza wachezaji wa timu ya Coastal Union baada ya kupanda daraja kucheza Ligi kuu msimu ujao katika halfa iliyofanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort Mjini Tanga kushoto ni Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union Steven Mguto na Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum
IMG_2380
 Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hemed Aurora
_MG_2226
Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Steven Mguto akizungumza katika halfa hiyo kushoto  ni Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa
_MG_2128
 Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union Juma Mgunda katika akiwa na Kocha wa Makipa Salim Waziri kushoto na kocha Msaidizi Joseph Lazaro kulia

_MG_2144
 Mfadhili wa timu ya Coastal Union Nassoro Binslum kushoto akisalimiana na mchezaji wa timu hiyo,Athumani Iddi Chuji
_MG_2150
Mfadhili wa timu ya Coastal Union Nassoro Binslum kushoto akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hemed Aurora
IMG_2242
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi tuzo Mchezaji Athumani Iddi Chuji ambazo zimeandaliwa na mfadhili wa timu hiyo ,Nassoro Binslum kwa ajili ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo baada ya kuipandishi timu hiyo kucheza Ligi kuu
IMG_2245
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akimkabidhi tuzo Mlinda Mlango wa timu ya Coastal Union Sharifu Kasilasi kwa mchango wao wa kusaidia timu hiyo kupanda daraja
IMG_2288
Kocha Msaidizi wa timu ya Coastal Union Joseph lazaro akipokea naye tuzo kutrokana na mchango wao waliuonyesha kwenye michuano ya Ligi Daraja la kwanza na kusaidia timu hiyo kupanda daraja(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
IMG_2289
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi tuzo Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union Juma Mgunda baada ya kufanikisha timu ya Coastal Union kupanda daraja

IMG_2283
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akimkabidhi  tuzo Kocha wa Makipa wa timu ya Coastal Union,Salim Waziri
IMG_2265
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi tuzo beki wa timu ya Coastal Union Hamad Juma
IMG_2348
Sehemu ya wachezaji wa timu ya Coastal Union wakiwa na wake zao wakipata chakula kwenye halfa hiyo
_MG_2108
Mwenyekiti wa Kamat ya Usajili ya Coastal Union Hemed Aurora kushoto akiteta jambo na Mwandishi wa Gazeti la Majira mkoani Tanga Mashaka Mhando
_MG_2123
Meneja wa Hotel ya Tanga Beach Resort Joseph Ngoyo akiteta jambo na mdau wa michezo wakati wa hafla hiyo ya kuwapongeza wachezaji wa timu
hiyo

_MG_2219
 Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Coastal Union Hemed Aurora katikati akiwa na Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Salim Bawaziri
_MG_2115
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Klabu ya Coastal Union,Hafidhi Kidoh kulia akisalimiana na mwandishi wa gazeti la Majira Tanga Mashaka Mhando kwenye halfa hiyo ya kupongeza wachezaji iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort Mjini Tanga
UONGOZI wa timu ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya” umetakiwa kushikamana na kutoruhusu migogoro na makundi yasiyokuwa na tija kwani yanaweza kukwamisha ndoto zao za kupata mafanikio katika msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania Bara.

Lakini pia waaache vurugu na chokochoko iwapo wanataka kupata mafanikio huku wakitakiwa kuangalie wale wachache watakaopelekea hali hiyo wasiwaunge mkono kwa kuonyesheni mfano wamewachoka.

Hayo yalibainishwa na Mfadhili wa timu hiyo,Nassoro Binslum wakati
akizungumza kwenye ghafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo sambamba na utolewaji wa zawadi baada ya kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort


Alisema tatizo kubwa ambalo limekuwa likirudisha nyuma mafanikio ya timu hiyo ni majungu,fitina na makundi ndani na nje ya timi hiyo hivyo ni
bora viongozi,wapenzi ,wanachama wakabadilika na kuongeza mshikamano

Binslum alisema umoja ulioonyeshwa na viongozi,wanachama na washabiki
wakati timu ilipokuwa inatafuta nafasi ya kupanda ligi kuu unatakiwa
uendelezwe ili uwe na tija kwa timu hiyo ili iweze kurudisha heshima
yake ya miaka ya nyuma kuchukua ubingwa.


Aidha alisema wakati timu zinapokuwa kwenye madaraja ya chini kunakuwa hakuna majungu wala makundi maana kipindi hicho hakuna udhamini wale fedha lakini inapopanda timu kila mtu anaweza kujitokeza kwa kueleza anaweza kuongoza.


“Ndugu zangu niwaambie tuwaache viongozi,benchi la ufundi na wadhamini
na sisi wengine tubaki tu kama wachezaji wa kumi na mbili kuisapoti timu
na tukifanya hivyo tutafanikiwa sana kwani tutakuwa tumeweka msingi
mzuri na imara “Alisema Binslum.


Kwa upande wake Mwenyekiti kamati ya usajili Hemed Aurora alisema mbali na mafanikio hayo jambo kubwa litakalozingatiwa kuhakikisha makundi hayatakuwa na nafasi ili kuepusha yaliyoikuta timu hiyo na kupelekea kushuka daraja.


Aurora alisema uwendeshaji wa timu unagharama kubwa itakayokuwepo si
kutafuta ubingwa wa ligi kuu bali kuhakikisha kunajengwa umoja utakaoleta mafanikio na kupambana na wale wasiokuwa na nia njema na timu hasa baada ya timu hiyo kupanda.


“Tunatambua sasa kazi ndio inaanza ni zaidi ya miaka 30 kihistoria tangu
timu hiyo iliptwaa ubingwa lakini ubingwa si kazi kama tutashikamana na
kuwapinga kwa pamoja wale maadui zetu wanaosubiri timu ipande waseme
timu yao tutawashughulikia  safari hii”Alisema.


Awali akizungumza  Mkuu wa Wilaya Tanga Thobias Mwilapwa  alisema timu kurudi kucheza ligi kuu kunafaida kubwa sana kwa wanamichezo tu ikiwemo wakazi wa mkoa huo kwani itasaidia kuinua ukuaji wa uchumi ndani ya Halmashauri ya Jiji.


Aidha alisema serikali iliahidi vitu vingi juu ya timu hiyo siku ya mapokezi yake ilipokuwa ikitokea Morogoro na jukumu lililopo ni utekelezaji wake ambao unaweza kuleta tija zaidi na timu nyingine kupanda na kufikia idadi kama ya zamani.


Hata hivyo alisema serikali imejitoa zaidi kuhakikisha inaisaidia timu
hiyo iweze kuwa tishio na kwenye michuano ya Ligi kuu msimu ujao huku
akizitaka zilizobakia nazo kuhakikisha zinaweka mipango imara ya kupanda
ili kukuza vipaji vya vijana wetu na uchumu wa pato mkoa kwa kupitia
michezo.


Kwa upande wake,Mwenyekiti wa timu hiyo,Steven Mguto alisema wataendelea kushikamana ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi kuu soka Tanzania Bara msimu ujao.


Aliongeza kuwa mshikamano waliouonyesha wakati wa michuano hiyo ya Ligi Daraja la kwanza wataendelea nao ili kuhakikisha wanarudisha enzi za
miaka 1988 walipotwaa ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages