Pages

PRECISION AIR YAONGOZA AFRIKA KWA KUFANYA SAFARI KW WAKATI 2017

Shirika la Ndege la Kitanzia Precision Air, limeshika nafasi ya kwanza Afrika kwa kufanya safari zake kwa kuzingatia muda.

Kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la Official Airline Guide (OAG) kwa kipindi cha Juni – Novemba 2017, Precision Air imeshika nafasi ya kwanza kwa kufanya safari kwa wakati dhidi ya mashirika mengine ya ndege 34 barani Afrika.

Ripoti hiyo inaonyesha Precision Air pia inaongoza katika ukanda wa Africa Mashariki kwa kufanya safari kwa wakati.

Katika kipindi kilichoripotiwa katika ripoti hiyo Precision Air ilifanya jumla ya safari 9,050 na kati ya hizo safari 8,672 zilifanyika kwa wakati, ikiwa ni 95.8%.

Mkurugenzi Mkuu wa Precision Air Bi. Sauda Rajab, akizungumzia ripoti hiyo amesema kuwa, Sababu kubwa y awatu kuchagua usafiri wa anga ni kuokoa muda.

“ Sisi Precision Air swala la kufanya safari kwa wakati ni kipaombele chetu kikuu.”

“Sisi Precision Air huesabu kuchelewa kwa ndege kuanzia dakika 0 baada ya muda wa safari kufika, hii ni kwa kuwa tumejizatiti kuhakikisha hatupotezi dakika hata moja ya mteja wetu.”

OAG ni shirika linatoa taarifa za kieletroniki za mashirika ya ndege pamoja na kutengeneza programu mbali mabli kwa ajili ya Mashirika ya ndege, Viwanja vya ndege, Taasisi za Serekali pamoja na mashirika mengine yanayo jihusisha na shughuli za usafirishaji. Shirika hili lina makao makuu yake nchini Uingereza.

Precision Air ni Shirika la Kitanzania lenye mtandao mkubwa zaidi wasafari Tanznaia, likifanya safari za ndani kwenda maeneo 12 na safari 2 za kikanda. Kutoka katika makao yake makuu Dar es Salaam Precision Air inafanya asafari kwenda Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Bukoba, Musoma, Kigoma, Tabora, Kahama, Mtwara, Zanzibar, Seronera, Nairobi, na Entebbe.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)