Duka la kisasa la Huduma kwa Wateja wa Tigo Wilayani Urambo |
Picha ya pamoja baada ya Uzinduzi wa Duka hilo |
Mmoja kati ya maafisa wa Tigo Bi.Tunu Kazinja akitoa maelezo kwa huduma ambazo wanazitoa mara baada ya uzinduzi wa Duka hilo la Kisasa wilayani Urambo. |
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Urambo wakipata maelezo ya huduma zinazotolewa na Kampuni ya Tigo katika moja ya Banda la maonesho wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi wa duka la Kisasa wilayani Urambo. |
Baadhi ya wananchi wa Urambo wakimsikiliza katibu tawala wilaya ya Urambo Bw.Paschal Byemelwa wakati akiwahutubia katika hafla fupi ya uzinduzi wa duka hilo la kisasa. |
Urambo, 12 Desemba, 2017- Katika mwendelezo wa harakati za kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanapata huduma bora kwa urahisi, kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tigo Tanzania leo imezindua duka kubwa la kisasa wilayani Urambo katika Mkoa wa Tabora.
Duka hilo jipya linapatikana katika mtaa wa Nsanjo, mkabala na depot ya Pepsi katika mji wa Urambo, lina uwezo wa kuwahudumia wateja zaidi ya 580,000 wa Tigo wanaopatikana wilayani hapo na viunga vyake.
Akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua duka hilo jipya la Tigo, Meneja wa Eneo la Ziwa wa Tigo, Gwamaka Mwakilembe alisema kuwa ufunguzi wa duka hilo jipya unaendana na mpango wa upanuzi na ukuaji wa kampuni hiyo ya simu unaolenga kuongeza idadi ya vituo vya huduma kwa wateja huku ikihakikisha kuwa bidhaa na huduma zote zinapatikana kwa urahisi na wateja wake nchi nzima.
‘Tigo imejizatiti kufanya uwekezaji utakaohakikisha wateja wetu wanapata huduma kwa viwango vya kimataifa ili waweze kupata suluhisho muafaka kwa mahitaji yao. Ufunguzi wa duka hili la kisasa mjini Urambo kunafanya idadi ya maduka yetu ya Tigo kufikia 15 katika Ukanda huu wa Ziwa, huku jumla ya maduka yetu yote ya Tigo nchini ikifikia 75,’ alisema.
‘Uzinduzi huu unaendana na sifa kuu ya Tigo kuwa mtandao unaowaelewa zaidi wateja wake na kuwapa bidhaa na huduma bora, za kibunifu, zinazoendana na mahitaji yao. Tunaendelea kuwekeza katika upanuzi na uboreshaji wa mtandao wetu wa simu, ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa sehemu ya mabadiliko na faida za ulimwengu wa kidigitali unaoongozwa na Tigo,’ Mwakilembe alifafanua.
Kwa upande wao, wakaazi wa Urambo wameelezea kufurahishwa kwao na ujio wa duka hilo jipya la Tigo kwani litawapunguzia adha ya kusafiri kwa mwendo mrefu kupata ufumbuzi wa matatizo yao ya simu pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za simu katika wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)