Meneja wa Njia Kuu za Umeme,Mhandisi Amos Kaihula akitoa mada katika mkutano wa wanakijiji cha Misigiri mkoani Singida
Mkuu wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida,Emanuel Luhahula akizungumza
Meneja wa Njia Kuu za Umeme,Mhandisi Amos Kaihula akizungumza na waandishi wa habari |
Meneja wa Njia Kuu za Umeme,Mhandisi Amos Kaihula akisisitiza jambo kwenye mkutano huo
WANANCHI wa kijiji cha Misigiri mkoani Singida wakifuatilia mkutano huo
Mmoja kati wa wananchi akiuliza swali katika mkutano huo
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Misigiri mkoani Singida wakifuatilia mkutano huo
WANANCHI wametakiwa kuithamini na kuitunza miundombinu ya umeme ambayo imewekezwa kwa fedha nyingi ili kuhakikisha wanapata wanapata uhakika wa huduma ya umeme katika maeneo yao yanayowazunguka.
Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida Emanuel Luhahula ambapo amesema kumekuwa na viashiria vya baadhi ya watu kuihujumu miundombinu ya umeme kwa maslahi binafasi jambo ambalo kufanya hivyo kunaathiri upatikanaji wa hudumaa hizo kwa wananchi.
“Lakini wanafanya hivyo bila kuthamini jitihada kubwa zinazofanywa na serikali …Hawa ni wanaoihujumu miundombinu ya umeme hawatavumiliwa hata kidogo kwa maana wanarudisha nyuma jitihada za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais JPM ambayo malengo yake makubwa ni kuinua uchumi wa wananchi kupitia viwanda ”Alisema.
Alisema viwanda hivyo vinategemea umeme na ndio maana serikali imeamua kuwekea kwenye nishati ya umeme hivyo watakaobainika wamehusika kuharibu miundombinu watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.
Aidha aliwaomba wananchi kushirikiana na serikali ikiwemo shirika la Tanesco kuhakikisha miundombinu ya umeme iliyopo kwenye maeneo yao inatunzwa sanjari na kuwafichua watu wote wenye nia ovu ya kurudisha nyuma maendeleo kwa kuihujumu.
Awali akizungumza Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Polisi (OCD) Bw Kimolo alisema kuwa kosa la uharibifu wa miundombinu ya umme ni sawa na lile la kuhujumu uchumi hivyo wananchi wasilichukulie kama jambo la mzaha.
Alisema uhujumu uchumi ni kosa kisheria hivyo wananchi wanapaswa kujihadhari na vitendo vya uvunjifu wa sheria kwani serikali ipo macho kwa kushirikiana na wananchi ili kuwafichua uhalifu huo.
Kwa upande wake akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Misigiri Mkoani Singida,Meneja wa Njia kuu za Umeme Mhandisi Amosi Kaihula alisisitiza suala la utunzaji wa miundombinu kuwa ni jukumu wananchi wanaoishi kwenye maeneo iliyopo kwani ni mali ya umma na shirika hilo limepewa dhamana ya kuisimamia.
“Ubadhirifu wa miundombinu hii una madhara makubwa ikiwemo kusababisha nchi kukosa umeme lakini pia kupelekea matatizo ya kukatikakatika kwa huduma hiyo kwenye baadhi ya maeneo jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya Taifa”Alisema.
Aliongeza licha ya kurudisha nyuma maendeleo lakini pia kusababisha kukosekana kwa huduma za kitabibu na kusimama kwa shughuli za viwanda unaosababishwa na ukosefu wa umeme baada ya miundombinu
kuhujumiwa.
Hata hivyo aliwataka wananchi kushirikiana kuitunza miundombuni ya umeme ikiwemo kuachana na tabia za kufanya shughuli za uchumi karibu na miundombinu ya umeme lakini wahakikishe wanachukua tahadhari wanapoona nyaya za umeme zimeanguka au kuwepo kwa hitilafu yoyote ili
kuepuka ajali za umeme. Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
kuepuka ajali za umeme. Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)