Msheli akizungumza na waandishi wa habari mapema katika uzinduzi wa mashindano hayo uliofanyika katika viwanja hivyo ambapo amewataka wachezaji wa Golf Nchini kujitokeza kwa wingi katika mashindano ya siku moja yenye lengo la kuenzi Uhuru wetu wa watanzania kutoka kwa wakoloniNia ya kuita mashindano haya Uhuru Cup ni kutaka kuenzi uhuru wetu kama watanzania ambao tulipa kutoka kwa wakoloni na ndio maana pia tukaamua kuyaweka siku moja baada ya sikukuu za Uhuru yaani tarehe tisa Desemba ili watanzania tukutane kwa pamoja kusheherekea sikukuu hiyo ya Uhuru wetu kwa kucheza na kutazama mashindano haya” Msheli
Kwa upande wa Nahodha wa Mchezo huo Japhet Masai alisema mashindano hayo yamejumuisha wachezaji wa kila rika na yamegawanyika katika vipengele vitano ambavyo yaani, Seniors, Ladies, Juniors,Cadies na Division Competition,
Masai aliongeza kuwa mchezo huu haulengi wakazi wa Dar es salaam pekee bali ni kwa mtanzania yeyote anayetaka kushiriki anaweza kujiandikisha na kupewa nafasi hiyo
Katika kuongeza chachu na hamasa kwa washindi, waandaaji wa mchezo huo wameandaa zawadi kwa washindi ikiwemo Baiskel, Simu za mkononi, Tv nk, ambazo zitatolewa kwa wachezaji watakaoibuka washindi kitika kila kipengeleMsheli aliongeza kuwa mashindano hayo hayataishia hapo tu bali yatakuwa endelevu kwa kila mwaka ili kuweza kuongeza hamasa kwa wachezaji wa mchezo huo
Wito umetolewa kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na kwa wapenzi wa Golf nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mashindano maalumu ya Golf yatakayo fanyika katika viwanja vya Lugalo Jijini Dar es salaam Wito huo umetolewa na Bwana William Msheli Mkurugenzi wa kampuni ya WIHAB GROUP kwa kushirikiana na EAG GROUP ambao ndio waandaaji wakuu wa Tamasha hilo la Uhuru Cup Open linalotarajiwa kufanyika tarehe 10/12/2017 siku ya jumapili katika viwanja vya Lugalo Jijini Dar es salaam Msheli alizungumza na waandishi wa habari mapema leo katika uzinduzi wa mashindano hayo uliofanyika katika viwanja hivyo ambapo amewataka wachezaji wa Golf Nchini kujitokeza kwa wingi katika mashindano ya siku moja yenye lengo la kuenzi Uhuru wetu wa watanzania kutoka kwa wakolon.Nia ya kuita mashindano haya Uhuru Cup ni kutaka kuenzi uhuru wetu kama watanzania ambao tulipa kutoka kwa wakoloni na ndio maana pia tukaamua kuyaweka siku moja baada ya sikukuu za Uhuru yaani tarehe tisa Desemba ili watanzania tukutane kwa pamoja kusheherekea sikukuu hiyo ya Uhuru wetu kwa kucheza na kutazama mashindano haya”
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)