Pages

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAVIPIGA JEKI VITUO VYA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU

 
 Mkurugenzi wa Msama Promotions,Bwa Alex Msama akishiriki kushusha vifurushi vya mchele,ambavyo baadae alivitoe kwa vituo vya watoto waishia katika mazingira Magumu,makabidhiano ya msaada huo yalifanyika kwenye ofisi zake Kinondoni jijini Dar.
 Mkurugenzi wa Msama Promotions,Bwa.Alex Msama akikabidhi zawadi ya vyakula kwa ajili ya sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha Mwandaliwa-Boko jijini Dar,Bi.Halima Mpeta. 

Kampuni ya Msama Promotions imetoa msaada wa vyakula mbalimbali  kwa baadhi ya vituo vya watoto waishio katika mazingira magumu,vilivyopo jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari wakati wa makabidhiano ya msaada huo,Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,Alex Msama alisema kuwa kama ilivyo ada ya kampuni yake,kila ifikapo mwishoni mwa mwaka hutoa sadaka kwa vituo mbalimbali vya watoto waishio katika mazingira Magumu.

"Nimeamua kufanya hivi pia kuwakumbuka wototo wetu wanaoishi katika mazingira magumu,na wao washerehekee sikukuu kwa furaha kama wenzao,kwa hiyo nimetoa unga,mchele,mafuta,viywaji mbalimbali na vingine ili watoto hao nao kwa pamoja wafurahie msimu wa siku kuu",alisema Msama.

Nae mlezi wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha Mwandaliwa-Boko jijini Dar,Bi.Halima Mpeta ameishukuru Kampuni ya Msama Promotions na Uongozi wake kwa kuwakumbuka katika msimu huu,wamemshukuru na kumuombea Heri zaidi afanikiwe katika mambo yake ili azidi kuwakumbuka na kuwasaidia wasiojiweza katika maeneo mbalimbali.

 Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama akimkabidhi msaada wa vyakula mmoja wa Viongozi wa kituo hicho cha watoto waishia katika mazingira Magumu cha Maunga,Kinondoni jijini Dar Es Salaamu.
Mwakilishi wa kituo cha TOVICHIDO,Bi Honoratha Michael akipokea msaada wa vyakula kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,Alex Msama ,hafla hiyo fupi ilifanyika ofisini kwake Kinondoni Jiini Dar

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)