Airtel Wababe wa Vifurushi vya Internet Kwa Sasa Tanzania - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Airtel Wababe wa Vifurushi vya Internet Kwa Sasa Tanzania


Meneja Masoko wa Kampuni ya simu za mkononi za Airtel Tanzania, Anneth Muga, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, leo mchana.

 Bando mpya za Smatika na Yatosha kutoka mtandao wa Airtel zikiwa splaid wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuonyesha ongezeko la GB na kwa bei nafuu tofauti na awali ikiwa ni pamoja na maboresho ya huduma UNI iliyo boreshwa na jinsi ya kuipata.

Siku za Hivi Karibuni Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania ilizindua kampeni yake Mpya ya SMATIKA ambayo kampeni hio imekuwa gumzo kutokana na Kuanzishwa kwa vifurushi vipya vya internet ambapo kwa sasa utapata mara mbili  zaidi kuliko awali. Kwa sasa Airtel wamewapa watumiaji wa simu za mkononi sababu za kutokuzima data kwa kuofia kuishiwa data sasa Ni mwendo wa Kuwasha data Muda wote.

Akizungumza katika mkutano huo Meneja Masoko wa Airtel, Anneth Muga,amesema kuwa Baada ya uzinduzi wa Bando la SMATIKA, baadhi ya wateja wameonekana kukwama kupata huduma za baadhi ya bando kama walivyozoea pamoja na kwamba kumekuwepo na matangazo ya mara kwa mara ya jinsi ya kupata huduma hizo na hasa bando la UNI.

Aidha, Anethy , amesema kuwa bando Mpya ya ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja kujichagulia bando la intaneti litakalompatia GB nyingi na muda wa maongezi wakati wowote, na kwa gharama nafuu ya hadi sh. 200 inayompa MB 40 ambayo haipatikani katika mtandao mwingine wowote.
 Meneja Uhusiano wa Airtel,  Jackson Mmbando ameongeza kufafanua kuwa kutokana na Airtel kutambua umuhimu wa matumizi ya Internet wameamua kuongeza ukubwa wa GB za matumizi ili kuwarahisishi wateja wao kufanya kazi bila hofu wala kubania DATA. ''Kwa sasa Bando mpya ya SMATIKA inampatia mteja GB 2 kwa siku saba kwa Sh. 5000, tofauti na ya awali iliyokuwa na GB 1, Sh. 10,000 zamani ulikuwa unapata bando la GB 2.5 kwa siku 7 mpya ya sasa unapata GB 6 kwa siku saba. amesema Mbando

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages