Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufungua mkutano wa WCF Arusha kesho - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufungua mkutano wa WCF Arusha kesho

 Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini (WCF) Abdulssalaam Omary ,kushoto kwake ni Meneja Matekelezo (WCF )Victor Luvena na wakwanza kulia ni Mkuu wa kitengo cha Uhusiano Laura Kunenge.picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog

Na.Vero Ignatus ,Arusha

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF )umeandaa mkutano wa siku mbili utakaoanza kesho Jijini Arusha katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni Mafaofidia:Haki ya Mfanyakazi na chachu katika uchumi wa Viwanda mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Kassim Majaliwa 

Akizungumza na waandishi wahabari Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini (WCF) Dr.Abdulssalaam Omary amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kutoa taarifa ya mwaka ya mfuko ,kutathimini maendeleo na changamoto zinazoukabili mfuko ,kupokea maoni ya kuboresha huduma za mfuko pia mada mbalimbali za uelimishaji zitatolewa na wataalamu mbalimbali wenye uzoefu kutoka baadhi ya nchi barani Afrika na kutoka Shirika la kazi Duniani (ILO) 

Hadi sasa Mfuko umekusanya zaidi ya shilingi milioni 800 kwa ajili ya matibabu kwa wanachama,hadi sasa taasisi 11,705 zimekwisha kujiunga na mfuko huo,2,105 bado hawajajiunga na mfuko huo wa fidia,ambapo Mkurugenzi Omary amesema kwa sasa wanajikita kutoa elimu kwa wafanyakazi waelewe kuhusiana na mfuko,wanatakiwa wafahamu kuwa kujiunga ni lazima  ili hapo baadae sheria itachukua mkondo wake.

Kwa upande wake Meneja matekelezo (WCF) Victor Luvena amesema kuwa Sekta za Umma pamoja na sekta binafsi zote zinatakiwa kujiunga katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi,waajiri wanatakiwa watume mchango wa wafanyakazi wao katika mfuko huo ambao ulianzishwa rasmi julai mosi 2015.

Ameeleza katika mkutano huo pamoja na mambo mengine ,mgeni rasmi atatunuku tuzo kwa waajiri waliofanya vizuri katika utekelezaji wa Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages