Mratibu wa Tamasha la watoto 'Baby Boxing Day 2017', na Mkurugenzi wa Linda Media Solution (LIMSO), Bi. Khadija Linda Kalili.
WAANDAAJI wa Tamasha la watoto litakalofahamika kwa jina la 'Baby Boxing Day 2017' wamewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini katika tamasha hilo ili kuweza kufanikisha hiyo ambayo imepangwa kufanyika Desemba mwaka huu (2017) Kibaha Mkoani Pwani.
Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari jana Mkurugenzi wa Linda Media Solution (LIMSO) ambaye pia ndiyo Mratibu tamasha hilo, Bi. Khadija Linda Kalili amesema kuwa siku hiyo itakuwa ni mahususi kwa ajili ya watoto kuanzia umri wa mwaka mwaka mmoja hadi umri wa miaka 17.
"Tunategemea kuwa na watoto wenye umri kunzia siku moja hadi miaka 17 ambao sharti kubwa la kuwepo katika eneo husika lazima kila mtoto aambatane na mzazi, mlezi au mwangalizi wake pia kutakuwa na ulinzi wa kutosha katika kamati ya maandalizi kwa watakaofika siku hiyo.
Aidha Kalili amesema kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na michezo mbalimbali ambayo watoto watafurahia kwa kuzingatia umri wao ikiwemo.
"Kwa mara ya kwanza Kibaha pamoja na viunga vyake nawaahidi kuandika historia mpya kutokana na kuwakumbuka watoto kwa aina katika siku hiyo, kwani hapo awali jamii imekuwa ikiwasahau watoto na kushindwa kuwakutanisha hasa katika kipindi hiki cha likizo.
"Tukumbuke watoto nao wanayo haki ya kukutana na kubadilishana mawazo kwani nao wanahitaji kukumbukwa katika masuala ya michezo na burudani hivyo kwa kulizingatia hilo tunatoa rai kwa wadhamini kujitokeza kufanikisha hili. LIMSO inawaahidi haitawaangusha," alisisitiza Bi. Linda Kalili.
Alisema ili kuleta upekee na mvuto wa siku ya tamasha wageni maalum waalikwa watakuwa ni watoto kutoka kwenye kituo kimoja wapo cha kulelea watoto yatima ambao watajumuika na wenzao siku hiyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)