Pages

TGNP Mtandao yakutanisha wenyeviti halmashauri na mameya

 
Ofisa Programu Uchambuzi na Machapisho wa TGNP Mtandao, Bw. Deogratius Temba akiwasilisha mada kwenye warsha ya baadhi ya wenyeviti wa halmashauri pamoja na mameya (hawapo pichani). Afisa Programu mwandamizi wa Ushawishi na utetezi wa TGNP Mtandao, Bi. Anna Sangai akiwasilisha mada kwenye warsha ya baadhi ya wenyeviti wa halmashauri pamoja na mameya (hawapo pichani). Baadhi ya washiriki kwenye warsha ya baadhi ya wenyeviti wa halmashauri pamoja na mameya wakiwa kwenye majadiliano kwenye vikundi. Mmoja wa washiriki kwenye warsha ya baadhi ya wenyeviti wa halmashauri pamoja na mameya akichangia hoja. Picaha ya pamoja ya baadhi ya washiriki wa warsha hiyo ya siku mbili.
TGNP Mtandao leo imefanya warsha na baadhi ya wenyeviti wa halmashauri pamoja na mameya lengo likiwa ni kujadili kwa pamoja changamoto anuai zinazoukumba mchakato wa bajati tangu ngazi za mitaa na vijiji.

Warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za TGNP Mtandao Mabibo jijini Dar es Salaam imeshirikisha viongozi hao kutoka Wilaya nane yaani Kishapu, Tarime, Morogoro Vijijini, Mbeya Vijijini, Kisarawe, Ilala, Ubungo na Kinondoni.

Akiwasilisha mada kabla ya majadiliano, Ofisa Programu Uchambuzi na Machapisho wa TGNP Mtandao, Bw. Deogratius Temba alisema washiriki watapata fursa ya kujadili mikakati na kuweka mipango ya namna ya kushughulikia masuala anuai ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia ili kuhakikisha masuala ya kijinsia yanapewa kipaumbele katika mipango na utekelezaji wa bajeti.

Alisema zipo changamoto mbalimbali ambazo zimeibuliwa kutokana na tafiti shirikishi ngazi za kijamii, yakiwemo masuala ya huduma zisizo ridhisha kwenye sekta ya afya, elimu, maji na maeneo mengine kama kilimo na uchimbaji ambapo watajadili na kushirikishana nini kifanyike kukabiliana na changamoto hizo.

Ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa sera kwa mrengo wa kijinsia inayofanywa na TGNP inawasaidia kupata taarifa zinazowawezesha kushauri watunga sera na wafanya maamuzi na wadau mbalimbali kuhusu masuala ya jinsia hususan kuziba mwanya wa kijinsia.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)