Pages

TAMWA Waanza maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia


Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga akizungumza leo na wanahabari akutoa kauli ya maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa chama hicho. Kushoto ni Ofisa Habari wa TAMWA, Happines Bagambi.


Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga akizungumza leo na wanahabari akutoa kauli ya maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa chama hicho. Kulia ni Afisa Mipango wa TAMWA, Strategic Manager.


Baadhi ya wanahabari na wasaidizi wa sheria ngazi za jamii wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga katika mkutano huo.


Baadhi ya wanahabari na wasaidizi wa sheria ngazi za jamii wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga katika mkutano huo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga akizungumza leo na wanahabari akutoa kauli ya maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa chama hicho. 


Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha CRC, Bi. Gladness Munuo (kulia) akitoa ufafanuzi kwa wanahabari katika mkutano huo.


CHAMA cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kimebaini kuwa matukio ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa chama hicho, kwa kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ubakaji kuwa bado ni changamoto, kwa kile kuendelea kushamiri ndani ya jamii.


Kwa mujibu wa taarifa ya TAMWA iliyotolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga amesema Kitengo cha Usuluhishi, CRC cha TAMWA kuanzia mwezi Januari hadi Agosti 2017 kimepokea kesi za ukatili wa kijinsia hasa ubakaji 57 tofauti na ilivyokuwa mwaka jana kwa kipindi hicho kupokewa kesi 9 tu.

Bi. Sanga alisema hali hiyo ya ongezeko inashamiriana na taarifa ya utendaji kazi ya Kituo cha One Stop Centre cha Hospitali ya Amana, Dar es Salaam ambapo imeonyesha kiwango cha matukio ya ubakaji kwa mwaka huu kiko juu kwa idadi ya watoto 141 waliochini ya miaka 18, huku watu wazima matukio kama hayo yakiwa ni 27 tu.

Alifafanua kuwa kuanzia Julai 2016 hadi Juni 2017 kituo hicho kilipokea jumla ya 420 huku matukio ya watoto yakifikia 316 sawa na asilimia 75 na watu wazima wakiwa 104 sawa na asilimia 25 ya ukatili wa kijinsia. 

"...Taarifa hiyo imeonesha idadi ya waliolawitiwa na kuripoti katika kituo hicho ni 44 sawa na asilimia 10.47 kati ya hao watoto ni 39 ukilinganisha na watu wazima ambao ni 5 kwa mwaka. Hali hii ya ukatili iko juu sana kwani watoto waliofanyiwa vitendo hivi wana uwezekano mkubwa wa kufanyia wengine katika kipindi cha makuzi yao.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA, Bi. Sanga aliongeza kuwa jukumu la ulinzi na malezi bora kwa watoto ni la jamii nzima wakiwemo marafiki, wazazi, ndugu, walezi, majirani na viongozi wakishirikiana na Serikali kuboresha na kusimamia utekelezaji wa sera na kubadilisha sheria kandamizi ili wahusika wa ukatili huu hasa kwa watoto wa kike wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.

Siku 16 ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa inayoongozwa na kituo cha Kimataifa cha wanawake katika uongozi tangu mwaka 1991 kutokana na mauaji ya kinyama ya akinadada wa Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominica 1960, Kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Funguka! Ukatili dhidi ya wanawake na watoto haumuachi mtu salama. Chukua Hatua'

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)