SHIRIKA LA MAENDELEO LA UJERUMANI 'GIZ' NA SHUWASA WAENDESHA WARSHA KWA WADAU WA MAJI MANISPAA YA SHINYANGA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

demo-image

SHIRIKA LA MAENDELEO LA UJERUMANI 'GIZ' NA SHUWASA WAENDESHA WARSHA KWA WADAU WA MAJI MANISPAA YA SHINYANGA

UF3A9563
Mshauri wa masuala ya Maji na Mazingira kutoka Shirika la Maendeleo la Ujerumani ‘GIZ’, Tina Eisele akielezea kuhusu mradi wa maji safi na mazingira katika maeneo ya wananchi wenye kipato cha chini unaotekelezwa na shirika hilo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA) katika kata ya Ndala na Masekelo manispaa ya Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefungua warsha ya wadau wa maji na mazingira katika manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani ‘GIZ’ kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA).

Lengo la warsha hiyo ni kuboresha huduma ya maji safi na usafi wa mazingira kwenye kata ya Ndala na Masekelo katika manispaa ya Shinyanga kupitia mradi wa huduma ya maji na usafi wa mazingira katika maeneo ya wananchi wenye kipato cha chini unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani ‘GIZ’ kwa kushirikiana na SHUWASA.

Akifungua warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga ambayo imekutanisha wataalamu wa maji na mazingira na viongozi kuanzia ngazi ya mtaa hadi mkoa,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wenye kipato cha chini.

Matiro alilishukuru shirika la GIZ kwa kushirikiana na SHUWASA kuanzisha mikakati ya kushughulikia changamoto za maji na mazingira katika kata ya Ndala na Masekelo wakishirikiana na wadau mbalimbali.

Alisema lengo la serikali ni kusimamia sera za nchi ili kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi na kwamba ipo tayari kushirikiana na wadau wote katika kukabiliana na changamoto zote zinazojitokeza.

“Mimi kama kiongozi mkuu wa wilaya hii,natoa shukrani za dhati kwa shrike la ‘GIZ’ kwa kuchagua mji wa Shinyanga kuwa moja ya miji mitatu nchini iliyopangwa kutekeleza mradi huu ikiwemo miji ya Korogwe na Dodoma,nawasihi kusimamia kikamilifu mradi huu ili uweze kunufaisha wananchi na pale mnapokwama msisite kuwasiliana na serikali”,alisema Matiro.

Naye Mshauri wa masuala ya Maji na Mazingira kutoka Shirika la Maendeleo la Ujerumani ‘GIZ’, Tina Eisele aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kuwaruhusu kutekeleza mradi huo ambao unatekelezwa katika maeneo ambako kuna wananchi wenye kipato cha chini.

Eisele alisema takwimu zinaonesha kuwa katika maeneo ambayo kuna wananchi wenye kipato duni,huduma za maji safi na usafi wa mazingira pia ni duni ndiyo maana wameamua kuanzisha mradi huo ambao utawalenga watu wenye kipato duni.

“Kupata maji safi na kuwa katika mazingira bora ni haki ya binadamu,tunataka maeneo yenye wananchi wenye kipato duni waangaliwe kwa jicho kama lile linalotumika kuangalia wananchi wenye kipato kikubwa,na hii ni miongoni mwa makubaliano ya mikataba mbalimbali ya kimataifa”,aliongeza Eisele.

Mkurugenzi wa SHUWASA,Injinia Sylivester Mahole alisema tayari mradi huo umeanza kutekelezwa huku akibainisha kuwa mradi huo utawanufaisha wananchi ambao walikuwa hawajafikiwa na huduma ya maji.

“Miongoni mwa changamoto katika utoaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira ni huduma kutowafikia wananchi wote na hivyo kusababisha makundi ya waliofikiwa na huduma na wasiofikiwa na huduma”,alieleza Injinia Mahole.

“Katika maeneo yanayotakiwa kupewa huduma kuna maeneo yanakaliwa na wananchi wenye kipato cha chini na hivyo kutokuwa na uwezo wa kuunganisha huduma za maji safi na usafi wa mazingira majumbani mwao,hivyo kwa kushirikiana na shirika la GIZ tumeamua kukabiliana na changamoto hii”,aliongeza Injinia Mahole.

Naye Mwezeshaji katika warsha hiyo,Injinia Mutaekulwa Mutegeki alisema kata za Ndala na Masekelo zitatumika kama mfano wa utekelezaji wa mradi huo ambapo pamoja na mambo mengine vituo vya kuchotea maji “Magati” vitajengwa kwenye maeneo hayo.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA WARSHA HIYO
UF3A9545Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefungua warsha ya wadau wa maji na mazingira katika manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani ‘GIZ’ kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA),katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga -Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
UF3A9532
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufungua warsha ya wadau wa maji na mazingira katika manispaa ya Shinyanga.
UF3A9522
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza wadau wa maji na mazingira kuhakikisha wanaungana katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi katika kupata huduma za maji safi na mazingira.
UF3A9538
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa SHUWASA ,Injinia Syliveter Mahole akifuatiwa na Erik Norremarle kutoka GFA.
UF3A9559
Mshauri wa msuala ya Maji na Mazingira kutoka Shirika la Maendeleo la Ujerumani ‘GIZ’, Tina Eisele akielezea kuhusu mradi wa huduma ya maji na usafi wa mazingira katika maeneo ya wananchi wenye kipato cha chini unaotekelezwa na shirika hilo katika kata ya Ndala na Masekeleo katika manispaa  ya Shinyanga kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA).
UF3A9561
Mshauri wa masuala ya Maji na Mazingira kutoka Shirika la Maendeleo la Ujerumani ‘GIZ’, Tina Eisele akiwasilisha mada kuhusu mradi huo wa maji.
UF3A9566
Mshauri wa msuala ya Maji na Mazingira kutoka Shirika la Maendeleo la Ujerumani ‘GIZ’, Tina Eisele akiendelea kuwasilisha mada ukumbini.
UF3A9590
Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada ukumbini.
UF3A9508
Mwezeshaji katika warsha hiyo,Injinia Mutaekulwa Mutegeki akizungumza ukumbini.
UF3A9534
Warsha inaendelea.
UF3A9535
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.
UF3A9536
Washiriki wa warsha wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
UF3A9554
Maafisa kutoka SHUWASA wakiwa ukumbini.
UF3A9593
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages