Pages

MUME WA IRENE UWOYA AFARIKI DUNIA

Taarifa iliyopatikana kutoka nchini Rwanda, inaeleza kuwa mume wa zamani wa Muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya, Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo, Ndikumana ambaye alikuwa kocha msaidizi wa timu ya soka ya Rayon Sports ambayo inaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini Rwanda, amefikwa na mauti hayo akiwa nyumbani kwake mjini Kigali. 

kwa mujibu wa Uongozi wa timu hiyo umesema kuwa jana Ndikumana ambaye alionekana kuwa bado yuko fiti na haonyeshi dalili zozote za kuumwa alifanya mazoezi na wachezaji wake na baadaye kuagana na kurudi nyumbane kwake, ambapo wamepatwa na mshtuko baada ya kusikia amefariki Dunia. Haijajulikana kifo chake kimesababishwa na nini kwani hakuwa mgonjwa na wala hajapata ajali. 

Mwili wake umepelekwa monchwari ya kiislamu ya dispensari ya Rwampala kwa maombi ya familia yake kwani miili ya waislamu haihifadhiwi katika monchwari za kawaida kwa mujibu wa imani zao. Uwoya na Ndikumana walifunga ndoa mwaka 2009 na kujaaliwa kupata mtoto mmoja aitwaye Krish kisha wakaja kutengana mwaka 2013. 

 Mungu ampe malazi mema peponi - Amin

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)