DKT. MWAKYEMBE AIPONGEZA PSPF KWA KUTWAA TUZO YA KIMATAIFA YA ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

demo-image

DKT. MWAKYEMBE AIPONGEZA PSPF KWA KUTWAA TUZO YA KIMATAIFA YA ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017

MWAKYEMBE_MAYINGU
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe, (kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, wakiwaonyesha waandishi wa habari, tuzo ambayo PSPF ilinyakua katika mashindano ya kimataifa wakati wa mkutano wa taasisi ya hifadhi ya jamii Duniani, International social security association, taasisi tanzu ya ILO, tuzo ya ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017 mjini Adis Ababa Ethiopia mwezi
uliopita. Tukio hili limefanyika pembezoni mwa mkutano wa kampeni ya uzalendo na utaifa iliyoongozwa na waziri Mwakyembe kwenye ukumbi wa mikutano wa PSPF jijini Dar es Salaam leo Novemba 25, 2017.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umenyakua tuzo ya kimataifa ya ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017, baada ya kuwa Mfuko unaotoa huduma bora kupitia ubunifu wa mafao ya muda mfupi, yaani service quality in short-term products.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuonyesha tuzo hiyo iliyokwenda sambamba na kampeni ya uzalendo na utaifa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu alisema, Mfuko huo unajivunia kwa kuwa Mfuko wa kwanza miongoni mwa Mifuko mitano ya Hifadhi ya Jamii nchini, kuanzisha bidhaa na huduma za muda mfupi ambazo zimekuwa kivutio kikubwa kwa wanachama na hivyo kuvutia mifuko mingine ambayo kwa sasa nayo
imeanza kutoa huduma hizo.
“Mwaka huu katika mkutano wake wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani yaani International Social Security Association, taasisi tanzu ya Shirika la Kazi Duniani,(ILO) imeipatia PSPF tuzo baada ya kuwa Mfuko bora barani Afrika katika utoaji huduma bora kupitia ubunifu wa Mafao ya muda mfupi yaani service quality kwenye short-term products.” Alifafanua Bw.
Mayingu.
Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe aliipongeza PSPF kwa kujinyakulia tuzo hiyo na kuliletea taifa heshima kubwa kimataifa.
“Kupambanishwa katika bara la Afrika na kushinda vigezo kadhaa ndipo unaambiwa bwana wewe unapata hii tuzo na tuzo hii imetolewa na taasisi yenye ushirikiano wa karibu sana na ILO hongereni sana.” Alipongeza Dkt. Mwakyembe.
Alisema ushirikiano wa karibu miongoni mwa wafanyakazi wa PSPF ndio umepelekea mafanikio hayo.
“Niwapongeze viongozi wote wa PSPF, Wafanyakazi wote wa PSPF, kwa kazi nzuri mnayoifanya mpaka mnatambuliwa na jumuiya ya Kimataifa.” Alisema.
Aidha kabla ya tukio hilo, Waziri aliwahamasisha watanzania kujenga moyo wa uzalendo na kujivunia utaifa wao kwani mambo hayo ni muhimu katika ujenzi wa taifa.
“Sisi tuliokuwepo kabla ya uhuru, niwaombe sana, tuwasaidie vijana wetu wa sasa kutambua tumetoka wapi, tuko wapi na tunaelekea wapi, kwa kujenga uzalendo wa kuipenda nchi yetu kama ambavyo ilikuwa hapo awali.” Alisema.


Kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muunganmo wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli baadaye mwezi ujao mjini Dodoma, na Waziri aliwahamasisha wadau mbalimbali kujitokeza na kuchangia fedha ili kufanikisha swala hilo muhimu kwa taifa.
5R5A6251
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyemba, akizungumza kuhusu umuhimu wa jamii kiujenga uzalendo wa taifa lao la Tanzania.
5R5A6007
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa, Leah Kilimbi, akizungumzia maudhui ya hafla hiyo.
5R5A6078
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. ASdam Mayingu, akizunhgumza kwenye hafla hiyo.
5R5A6104
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza wakayti wa hafla hiyo.
5R5A6060
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ambaye pia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Lulu Mengele, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw.Sami Khalfan, wakifuatilia hafla hiyo.
Nelly+Msuya-dawasco
Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Nelly Msuya akizungumza kwenye hafla hiyo.
5R5A6235
Mkurugenzi wa vipindi wa Azam TV, Bw. Charles Hillary, (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
5R5A6185
Bw. Mayingu akizungumza huku akipongezwa kwa makofi na waziri Mwakyembe na Bi.Joyce Fisso, Katibu Mtendaji bodi ya Filamu Tanzania.
5R5A5972
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bi. Grace Michael Kisinga.
5R5A6171


5R5A6226


5R5A6243
Baadhi ya wageni waalikwa
5R5A6180
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fisso, akizungumza.
5R5A6252
Baadhi ya wasanii waliohudhuria hafla hiyo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages