WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2017: PSPF YATEMBELEA WATEJA MAJUMBANI, NIA NI KUWAJULIA HALI NA KUWAHAKIKI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2017: PSPF YATEMBELEA WATEJA MAJUMBANI, NIA NI KUWAJULIA HALI NA KUWAHAKIKI


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
Wakati Wiki ya Huduma kwa Wateja ikiendelea kote Duniani, Mfuko wa Pensheni wa PSPF, umeitumia wiki hiyo sio tu kwa kuhudumia wateja ofisini bali pia kutoka nje ya ofisi na kuwatembelea Wanachama na Wastaafu wa Mfuko huo  majumbani kwao.

Mmoja wa waiotembelewa ni Mstaafu Bw. Kassim Salehe Mafanya,(63), anayeishi Kipunguni B, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kitendo ambacho kilimfurahisha sana. Kaimu Mkurugenzi Mkuu, wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa akifuatana na timu yake, Oktoba 4, 2017 alifika nyumbani kwa Bw. Mafanya, na kufanya mazungumzo naye ikiwa ni pamoja na kumpatia fomu ili aijaze kwa nia ya kumuhakiki kama ambavyo sheria inataka.

Kwa mujibu wa Sheria, Mstaafu anatakia kufika kwenye ofisi za PSPF kuhakikiwa kila mwaka ili kujua uwepo wake, anasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa “Kama mnavyofahamu wiki hii ni wiki ya huduma kwa wateja Duniani kote, na sisi PSPF kupitia ofisi zetu nchi nzima tunajitoa na kutembelea wateja wetu ambao ni pamoja na wanachama na wastaafu, na leo tuko hapa eneo la Kipunguni B, tumekuja kumtembelea Bw. Kassim Salehe Mafanya, ambaye ni mstaafu na lengo ni kumjulia hali na kumuhakiki uwepo wake kama ambavyo sheria inataka.” Alisema.
Afisa Uendeshaji wa PSPF ambaye pia alifuatana na Bw. Mkangaa, alimsomea Mstaafu huyo, maelezo yaliyomo kwenye fomu ya uhakiki kabla hajaweka saini kenyefomu hiyo.

Aidha kwa upande wake, Mstaafu huyo Bw. Mafanya aliishukuru PSPF kwa kitendo hicho cha kuwatembelea wateja wao yeye akiemo na kwamba ni kitendo kinachofaa kupongezwa. “Siku ya leo nimefarijika sana, kwanza sikutegemea kama nigepokea ugeni kama huu kutoka PSPF wa kunitembelea mimi Mstaafu hapa nyumbani kwangu,” Alianza kwa kusema Bw.
Mafanya wakati akiwakaribishas viongozi hao wa PSPF.“Kitendo
cha kuwakumbuka wastaafu kama sisi na kuwatembelea majumbani kwao kimenifurahisha sana na niwapongeze kwa tabia hiyo, Alisema.
Bw. Mafanya alimuhakikishia Kaimu Mkurugenzi Mkuu, kuwa amekuwa akipokea pensheni yake kila mwezi na bila matatizo yoyote na amekuwa akipata ushirikiano mzuri kutoka kwa maafisa wa PSPF kila anapokwenda kufuatilia pensheni yake.

“Nashukuru pensheni yangu inaendelea vizuri, huu ni mwaka wa 14 tangu nistaafu, nachukua vizuri tu pensheni ya kila mwezi na uzuri nikwamba inaboreshwa, na ndio maana mpaka hivi sasa tunaonekana tuna afya nzuri na ninaendelea na shughuli zangu mimi na familia yangu.” Alipongeza.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa, (kushoto), na Mteja wa PSPF, ambaye ni Mstaafu, Bw. Kassim Salehe Mafanya, (63), wakifurahia jambo wakati kiongozi huyo wa alipomtembelea Mstaafu Mafanya nyumbani kwake Kitunda B, nje kidogo ya jiji Oktoba 4, 2017 wakati Dunia ikiadhimisha Wiki ya Huduma Kwa Wateja.
Bw. Mafanya, (kulia), akipokea fomu hiyo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa,  (kushoto), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi,  wakishuhudia Bw. Mafanya akijaza fomu ya uhakiki ya Mstaafu, kutoka PSPF hapo nyumbani kwake.
Bw. Mkangaa, (Kushoto), akipeana mikono na Bw. Mafanya baada ya kumtembela nyumbani kwake.
Bw. Mkangaa akisalimiana na familia ya Bw. Mafanya
Bw. Mkangaa akiwa amembeba mjukuuu wa Bw. Mafanya.
Bw. Mafanya (kushoto), akifurahia jambo na Afisa Uendeshaji kutoka PSPF, Bw.Ernest Massay
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, na timu yake akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafamilia wa Bw. Mafanya mbele ya nyumba yake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages