Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola ameitaka jamii kujenga tabia ya kutunza mazingira katika maeneo yao kwa faida ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.
Katibu mkuu Profesa Kamuzola ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akifunga mafunzo ya mradi wa uchumi wa kijani chini ya Jangwa la Sahara, yaliofanyika jijini Tanga.
Alisema kuwa ni vyema wananchi wakajua umuhimu halisi wa kutunza mazingira na kuyatumia katika kujiongezea kipato.
Mradi wa uchumi wa kijani chini ya Jangwa la Sahara ulikuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya ushirikiano wa kimtaifa KOICA chini ya Programu ya UNESCO.
Kwa upande wake Katibu tawala wa mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi ameisisitiza jamii kupokea vizuri miradi wanayokuwa wakiletewa na wafadhili ili iwaongezee kipata na elimu zaidi katika utunzaji wa mazingira.
"Wananchi ni vyema mkabadirika na kuacha kuishi bila kutambua kuwa mazingira ukiyatunza yanakuletea kipato cha juu kabisa, ukiangalia unaona unaweza kutengeneza mkaa kwa kutumia magunz ya mahindi baada ya kuwa umeshavuna hiyo ni faida tosha kabisa," alisema Mhandishi Zena Saidi.
Naye Mhifadhi wa Mazingira ya asili ya Amani, Bi. Mwanaidi Kijazi aliwashukuru sana wafadhili wa mradi huo kwa kuweza kutoa elimu kwa wananchi ... elimu ambayo imekuwa endelevu na kuwazalishia kipato cha hali ya juu.
Bi. Mwanaidi alisema kuwa wananchi baaada ya kupewa elimu wameweza kujiendeleza katika miradi mbali mbali ikiwemo kutengeneza mkaa kwa kutumia majani ya mimea/magunzi, ufugaji wa vipepeo ambao wamekuwa wakiwazalisha kwa kutengeneza mapambo, kilimo cha uyoga, kilimo cha asali.
Hifadhi ya mazingira ya amani inaendeleza ikolojia na bioanuwai ambazo ni adimu duniani na zinapatikana katika milima ya usambara mashariki, na ina jumla ya vijiji 72.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)