Afisa mtendaji wa kata ya Ng’ang’ange bwana Aron Mwenzegule akiwa mjumbe wa mkutano mkuu taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Gervas Kahemela wakibadilisha mawazo wakati wa ziara ya kutembelea shule ya msingi Mdeke
Mwalimu mkuu wa shule ya Mdeke Pascal Aloyce akizungumza mbele ya wajumbe wa chama cha mapinduzi wakati wa ziara ya kubaini changamoto za shule hiyo
Mjumbe wa mkutano mkuu taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Gervas Kahemela akiwa makini kusikiliza anachoambiwa na mwalimu wa shule ya msingi Mdeke wakati wa ziara yake katika shule hiyo.
Na Fredy Mgunda,Kilolo.
Shule ya msingi ya Mdeke iliyopo kata ya Ng’ang’ange wilayani kilolo ina walimu 6 wanaowafundisha zaidi ya wanafunzi 440 na kusababisha kutotolewa kwa elimu bora kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.
Hayo yamebaini wakati wa ziara iliyofanywa na wajumbe wa kati za siasa wa chama cha mapinduzi (CCM) wilayani kilolo walipokuwa wameenda kwa lengo la kufanya usafi katika kata ya Ng’ang’ange
Akizungumza mara baada ya kumaliza kufanya usafi mwalimu mkuu wa shule ya Mdeke Pascal Aloyce alisema kuwa shule inajumla ya walimu 9 lakini walimu walimu watatu wameenda kusoma hivyo walimu waliopo shuleni ni walimu sita na kusababisha ugumu wa kuwafundisha wanafunzi wa shule hivyo.
“Tuna jumla ya wanafunzi 448 na walimu tupo 6 sasa utaona kiasi gani tunapata ugumu wakufunzisha wanafunzi na kuwapa elimu bora kwa kuwa walimu tumezidiwa na idadi ya wanafunzi huku walimu wengine wakifundisha masomo ambayo hawayawezi vizuri” alisema Aloyce
Aloyce alisema kuwa licha ya kuwa kuna walimu sita lakini walimu wawili wanafundisha elimu ya awali na walimu wanne ndio wanafundisha kuanzia darasa la kwanza hadi la saba hapo ndio utakundua kiasi gani kazi ya ualimu katika shule hii inakuwa ngumu.
“Ukiangalia tuna madarasa saba hivyo walimu wanne tu ndio tunafundisha hapo utaona kwa kiasi gani tunapata ugumu wa kufundisha na kuwapa elimu bora wanafunzi wetu hivyo tunawaomba mtufikishie kilio chetu huko juu ili kuweza kutatua tatizo hili” alisema Aloyce
Aidha Aloyce alisema kuwa walimu wa shule hiyo wamekuwa wakijitoa kufundisha kwa jitihada zao zote na kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi wanasoma katika shule hiyo licha ya kuwa na changamoto lukuki.
“Ukingalia mwaka huu tulikuwa na wanafunzi 53 na waliofaulu ni wanafunzi 40 hivyo utagundua kwa kiasi gani sisi walimu wa shule hii tunahitaji pongezi kwa kazi tunayoifanya licha ya changamoto zinazotukabili walimu wa shule hii ya Mdeke” alisema Aloyce
Lakini Aloyce alisema kuwa walimu wanakumbana na changamoto ya nyumba za walimu hivyo inawalazimu walimu kuishi umbali wa zaidi ya kilimeta mbili hadi ufike shule hivyo utaona kuwa walimu mara kwa mara wanafika shule wakiwa wameshachoka na kuathiri swala la ufundishaji wanafunzi.
“Mwalimu anatoka mbali sana sasa unafikiri mwalimu huyo akifika shule inakuaje hivyo na hii changamoto tunaomba mtupelekee huko kwa viongozi wa ngazi za juu mfano tunawalimu anayenyonyesha hebu angalia mwalimu hadi anyonyeshe unafikiri atafika shule saa ngapi tatizo la nyumba ni kubwa sana” alisema Aloyce
Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo Saidi Kiponza alisema kuwa wameziona changamoto zilizopo katika shule hiyo na kwenda kuzifikisha kwa viongozi wa ngazi za juu ili kuweza kuzitafutia ufunzi na kwafanya wafanyakazi wa serikali kuitekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kikamilifu.
“Sisi hatujaja kwa maonyesho tumekuja kufanya kazi na kuhakikisha viongozi wa serikali wanaitekeleza vilivyo ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi 2020 ili chama hiki kiendelee kuwa madarakani miaka yote” alisema Kiponza
Naye mjumbe wa mkutano mkuu taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Gervas Kahemela alisema kuwa lengo la ziara hiyo katika kata ya Ng’ang’ange ni kufanya usafi na kubaini changamoto zinazowakabili wananchi na kuzipeleka kwa viongozi wa serikali kuzitafutia ufumbuzi wa changamoto ambazo tunakuwa tumezibaini na kuzitatua.
“Unajua ukujua eneo gani kunachangamoto gani inakuwa kazi rahisi sana kuzitafutia ufumbuzi mapema na kuwafanya wananchi waendelee kukiamini chama cha mapinduzi kwa kazi yake inayofanywa chini ya Rais wetu Dr John Pombe magufuri kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo” alisema Gervas Kahemela.
Usikose kutembelea blog hii kwani bado kuna habari ya kuhudhunisha kutoka katika shule hii ya Mdeke ilyopo wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)