Pages

NCHI ZILIZOENDELEA KITEKNOLOJIA ZISAIDIE KUBORESHA HARAKATI ZA UCHUMI WA VIWANDA-SAMIA

Nchini zilizopiga hatua katika maendeleo ya Sayansi na Teknolojia zimetakiwa kuwa tayari kusaidia kuleta teknolojia hiyo ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza za kimazingira katika harakati za kufikia maendeleo ya uchumi wa viwanda.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya 72 ya Umoja wa Mataifa (UN) na wageni waalikwa kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassani amesema kwamba maendeleo ya viwanda yanakwenda sambamba na tishio la uharibifu wa mazingira na tabianchini ni muhimu kwa wadau wote wa maendeleo kujipanga.

“Sote tunajua kwamba maendeleo ya viwanda yalikuja na uharibifu mkubwa wa mazingira na hali ya hewa katika kipindi cha mapinduzi ya viwanda kipindi kile cha karne ya 18th na 19th sasa ni muhimu kwa mataifa yaliyopiga hatua za kisayansi na teknolojia kuweza kuwa tayari kusaidia kwenye hili,” amesema Makamu wa Rais.

Amesema nchini juhudi zinaendelea za kukuza uchumi na maendeleo ya watu lakini ni muhimu kwa wananchi kwa ujumla wao kuweza kulinda na kuhifadhi zaidi maliasili, hifadhi na rasilimali za taifa ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez mara baada ya kuwasili kwenye maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kwamba ofisi yake ambayo inashughulikia mambo ya tabianchini na mazingira wametunga sera, sheria na sera mpya ya mazingira na uendeshaji wa mambo ya mazingira pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016 ambapo ni kuhakikisha juhudi za viwanda haziwezi kuathiri mazingira ya nchini.

Awali akihutubia hadhara hiyo, Makamu wa Rais alifafanua kwamba kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya Umoja wa Mataifa (UN) ni kwamba “Maendeleo ya viwanda na utunzaji wa mazingira kwa maendeleo Endelevu” ni sahihi kwa wakati muafaka katika juhudi za kuibadilisha Tanzania kufikia uchumi wa viwanda.

Amesema kwamba ni takribani miaka miwili tangu kuanzishwa kwa agenda za maendeleo endelevu 2030, ambapo malengo 17 yamewekwa na Tanzania imefanikiwa kuingia kwenye awamu ya pili ya maendeleo endelevu katika juhudi za kupambana na umasikini.

“Katika kuhakikisha serikali inakuwa na fedha za kutosha kufikia malengo hayo ya maendeleo chini ya utawala wa Dkt John Joseph Pombe Magufuli mapambano dhidi ya rushwa, matumizi mabaya ya fedha za umma, ujangili na ubadhilifu yanadhibitiwa kikamilifu na mapambano yanaendelea,” alisisitiza. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki na Afisa Mwakilishi wa Unesco Dar, Ann Therese Ndong- Jatta mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee kushiriki maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa.

Kwa upande wake, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini (UN) Alvaro Rodriguez aamesema kwamba bado wanakabiliwa na changamoto nyingi hasa upande wa rasilimali ila wana matumaini kwamba kwa pamoja wanaweza kuwashawishi wadau wa maendeleo kusaidia katika vipaumbele vya nchini.

“Wakati ambapo Tanzania inafanya mageuzi makubwa, inapoelekea kuwa nchini ya hadhi ya kipato cha kati, msaada wa Umoja wa Mataifa (UN) hauna budi kuendana na mahitaji na changamoto mpya,” amesema Rodriguez

Aliongeza pia kwamba Umoja wa Mataifa (UN) wataendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na wadau wengine wa maendeleo ili kuweza kufikia malengo 17 ya maendeleo endelevu na aliishukuru Tanzania kuendelea kupokea wakimbizi pamoja na changamoto nyingi za kuhifadhi wakimbizi hao.

Maadhimisho ya Umoja wa Mataifa (UN) kufanyika kila mwaka katika kukumbuka tangu umoja huo uanzishwe mwaka 1945 na Tanzania ilijiunga kwa mara ya kwanza mwaka 1961 mara tu baada ya uhuru na sherehe hizo za jana zilihudhuriwa na wageni mbalimbali mawaziri, mabalozi, viongozi wa dini na zilipambwa na bendi ya Jeshi la Watanzania wa Tanzania (JWTZ).

Na Damas Makangale wa Thebeauty Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwakilishi wa UNFPA nchini, Jacqueline Mahon mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwakilishi wa UNICEF nchini, Maniza Zaman mara baada ya kuwasili katika maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akipokea heshima katika maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride la heshima katika maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga pamoja na 10) Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez wakishuhudia bendera ya Umoja wa Mataifa ikipandishwa kuashiria kilele cha maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja huo. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga akiazungumza machache kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) kuzungumza kwenye maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akihutubia hadhara ya wageni mbalimbali (hawapo pichani) na kusisitiza umuhimu wa teknolojia katika kufikia uchumi wa viwanda wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa kwenye maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa huo yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi tuzo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan ya heshima kwa kutambua ushirikiano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja huo. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi tuzo ya heshima Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja huo. Pichani juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, viongozi wa Serikali pamoja na wadau wa maendeleo waliohudhuria sherehe za miaka 72 ya Umoja wa Mataifa.


Wanafunzi wa shule ya sekondari Weruweru wakitoa burudani kwa vitendo kwenye maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja huo.
Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na wakuu wa mashirika yaliyochini ya Umoja wa Mataifa nchini wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja huo. Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja wanafunzi wa shule ya Sekondari Dodoma, Weruweru na Zanzibar. Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje katika picha ya pamoja. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiagana na baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 72 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)