Pages

KAMPUNI YA UDHIBITI WA BIDHAA , KUMLINDA MTEJA YAZINDULIWA TANZANIA

Na Dotto Mwaibale

Kampuni ya Sproxil inayoongoza dunian, inayotumia teknolojia ya simu za mikononi kudhibiti bidhaa bandia na kumlinda mteja, imezinduliwa nchini Tanzania.

Sproxil Tanzania inayowezeshwa na mfuko wa maendeleo ya ubunifu wa bidhaa za binadamu duniani (Human Development Innovation Fund (HDIF), imewasilisha ubunifu bora wa namna ya kudhibiti bidhaa bandia/ batili kwa makampuni, taasisi, za udhibiti, serikali na kuwezesha majadiliano ya wazi kwa ushirikiano wa karibu ili kudhibiti bidhaa bandia.

Majadiliano hayo yamefanyika leo Oktoba 26, 2017 jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, TFDA, TBS, Tume ya Ushindani, Wafanyabiashara
na wadau wengine kutoka sehemu  mbalimbali pamoja na waandishi wa habari.

Licha  ya  kuzindua  huduma ya udhibiti  wa bidhaa batili ili
kulinda makampuni  ya Tanzania, vilevile Sproxil inachukua fursa hii  kama
jukwaa  maalumu kuweka wazi na kueleza ushirikiano kati ya wadau wote katika suala zima la udhibiti wa bidhaa bandia na nafasi ya watumiaji wa bidhaa hizo.

Aidha, kuwasilisha taasisi za kudhibiti na kutakuwa na zoezi la kuthibitisha ubora  wa bidhaa chini ya usimamizi wa Bodi ya Viwango vya Ubora Tanzania (Tanzania Bureau of Standards), na ile ya bodi ya utawala wa bidhaa za chakula na udhibiti wa madawa nchini Tanzania (Tanzanian Food & Drug Authority ) na jopo la wawakilishiwa wa sheria, wakurugenzi, kutoka sekta binafsi waliochaguliwa kuwasilisha matakwa ya sekta binafsi kwa ujumla wake.
 Akizungumzia umuhimu wa uzinduzi huu kwa jamii ya Watanzania kwa ujumla, Mkurugenzi Mkuu wa Sproxili Afrika, Chinedum Chijioke alisema;
“Bidhaa bandia, batili, haramu au zilizo chini ya kiwango ni hatari kwa afya za watumiaji wasio na hatia, upotoshaji wa ubora wa bidhaa na pia zinateremsha ubora na mwelekeo wa kiuchumi.

Uwepo wa bidhaa bandia na zisizo na sifa zinaathiri vibaya watumiaji na kuathiri sifa za wazilishaji ndiyo sababu imekuwa wajibu wa serikali na sekta binafsi kuwawezesha Watanzania kutumia njia bora au zilizo chini ya udhibiti zinazoratibiwa na Kampuni ya Sproxil." 
 Kwa upande wake, David McGinty ambaye ni nahodha wa timu ya HDIF Tanzania amesema;

"Teknolojia ya kumlinda mteja ya Sroxil ni nzuri na ni mfano bora wa ubunifu, ina vipimo sahihi na ina ubora wa mawasiliano  (1CT4D) ambayo tunaamini inaweza kufanikisha malengo yaliyokusudiwa kwa jamii ya watumiaji bidhaaa."

Udhibiti wa ubora wa bidhaa kwa wataalam wa Sproxil unaweza kutumiwa na bidhaa kutoka sekta yoyote kwa kutumia simu, Watanzania sasa wanaweza kudhibiti na kupima ubora wa bidhaa kwa muda mfupi kwa kutumia ujumbe mfupi wakitumia namba maalum kwenda kwenye vifaa maalum vilivyo katika mtandao wa Sproxil kuhoji na kuthibitisha haraka ubora wa bidhaa.

Tangu huduma hii ya udhibiti ubora ilipozinduliwa mwaka 2010, Sproxil imeweza kudhibiti zaidi ya bidhaa milioni 50 kupitia wateja waliohoji ubora wake duniani kote na hii ni idadi kubwa kabisa ya kesi hizi kuripotiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika majadiliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye alisema anaikaribisha Kampuni ya Sproxil nchini kwani ni fursa ya pekee kwa walaji itakayowawezesha kutumia simu zao za kiganjani kubaini bidhaa bandia zikiwemo mbegu na mbolea kwani huko ndiko kuna mbegu feki nyingi.

"Mimi naona ni fursa ambayo imekuja kwa Watanzania itakayotusaidia na watakaoumia ni wale wanaotengeneza vitu feki, nawakaribisha sana kwa uwekezaji wao ambao una faida kwetu," alisema Simbeye.
 Kuhusu Sproxil Sproxil® inatumia tekinolojia ya simu  na ugunduzi wa uhalifu  kudhibiti udanganyifu ili kuthibitisha ubora wa bidhaa ambazo zitawafaa wateja duniani kote.
 Ufumbuzi wa bidhaa bora unaotumiwa na Sproxil umekuwa ukitumiwa na watenegnezaji bidhaa wa kimataifa na bidhaa bora katika viwanda vyote kudhibiti usambazaji wa bidhaa haramu, kusambaza taarifa za kweli kwa bidhaa halali na bora, na utumiaji wa fedha kwa bidhaa zilizokusudiwa kununuliwa kwa matumizi muafaka. Ikiwa na timu yake ya wataalamu
waliotapakaa barani Afrika, Asia na Amerika, Sproxil imeweza kufanya kazi kwa ufanisi katika mabara yote matano na kutoa huduma kwa zaidi ya nchi 100 duniani kote. Sproxil ni kampuni pekee inayojali mteja na kulinda bidhaa chini ya ISO 9001 na vyeti vya ubora vinavyotolewa na ISO 27001. Kwa maelezo zaidi na  bidhaa za  Sproxil, tafadhali tembelea  tovuti ya www.sproxil.com.
 Washiriki wakichangia mada.
Washiri wakishuhudia uzinduzi huo. PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)