NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA NISHATI SUBIRA MGALU AWAHAKIKISHI WAKAZI WA MBAGALA UMEME WA UHAKIKA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA NISHATI SUBIRA MGALU AWAHAKIKISHI WAKAZI WA MBAGALA UMEME WA UHAKIKA

Mhandisi Emanuel Manlabona  akimuonyesha  Naibu Waziri Nishati Subira Mgalu Juu ya uwezo wa kituo  hicho cha kusambaza umeme kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Usafirishaji  Umeme Mhandisi Bishaija Kahitwa
Mhandisi Emanuel Manlabona akimuonyesha  Naibu Waziri Nishati Subira Mgalu Juu ya uwezo wa kituo hicho cha kusambaza umemekulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Usafirishaji Umeme Mhandisi Bishaija Kahitwa
Naibu  Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu kulia akisalimiana na mkazi wa Mbagala Naibu  Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu amewahakikishia wakazi wa Mbagala umeme wa uhakika  kwani wizara  ya nishati kwa kushirikiana na  wataalamu mbalimbali wa TANESCO  wanafanya jitihada za kutosha kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana  ili kuwezesha matumizi ya viwanda mbalimbali vilivyopo mbagala na matumizi 
ya Nyumbani kwa wakazi wa mbagala.

“Tumesikia matatizo yenu yanayohusiana na Umeme,  ila Napenda kuwahakikishiani kuwa  Wizaraya Nishati pamoja na  TANESCO kwa ujumla tunafanya kazi, kuhakikisha umeme mbagala unakua  wa Uhakikia, leo hapa nimekuja kutembelea hiki kituo cha usambazaji  umeme cha mbagala , ambacho kinajengwa na kwa kushirikiana kwa pamoja,  tunapambana kituo hichi kikamilike ndani yam waka huu mpaka kufikia  disemba , kituo hichi kiwe kimekamilika. “

Hayo aliyazungumza  jana katika ziara aliyoifanya  katika  vituo vya kusafirisha umeme, kituo cha mbagala na kurasini  lengo kubwa ikiwa ni kuangalia hali halisi ya utendaji wa TANESCO katika  kuhakikisha wananchi wanapata huduma hii ya Nishati ya umeme wa Uhakika. 
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages