Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (kulia) akizungumza na wanahabari leo Dar es Salaam, alipokuwa akitoa utabiri wa mvua za msimu wa mwezi Novemba 2017 hadi mwezi Aprili 2018 ikiwa ni kwa mara ya kwanza TMA kutoa utabiri huo. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (katikati) akizungumza na wanahabari leo Dar es Salaam, alipokuwa akitoa utabiri wa mvua za msimu wa mwezi Novemba 2017 hadi mwezi Aprili 2018 ikiwa ni kwa mara ya kwanza TMA kutoa utabiri huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa TMA na Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa pamoja na Mkurugenzi Matumizi ya Hali ya Hewa, Dk. Ladslaus Chang’a.
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo imetoa utabiri kwa mara ya kwanza wa mvua za msimu wa mwezi Novemba 2017 hadi mwezi Aprili 2018 ikiwa ni maeneo mahususi ambayo hupata mvua kwa msimu mmoja kwa mwaka.
Akitoa utabiri huo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi alisema mwelekeo wa mvua za msimu kwa maeneo hayo unatarajiwa kuwa wa wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Dodoma, Singida, Kigoma, Tabora, Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Ruvuma, Lindi na Mtwara pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro.
Alisema mvua katika maeneo ya mikoa ya Kigoma, Tabora, Rukwa, Katavi, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Lindi, Mtwara na kusini mwa mkoa wa Morogoro zinatarajiwa kuanza kunyesha wiki ya kwnza ya mwezi Novemba 2017 na kusambaa katika mikoa ya Dodoma na Singida ndani ya wiki ya kwanza ya Desemba 2017.
Dk. Kijazi aliongeza kuwa mtawanyiko hafifu wa mvua pia unatarajia kujitokeza katika maeneo ya mikoa ya Lindi na Mtwara kipindi cha Januari hadi Februari, 2018, kipindi ambacho alisisitiza ukanda wa mvua unatarajiwa kuwa nje ya eneo la kusini mwa Tanzania. "...Mvua zinatarajiwa kuisha katika wiki ya mwisho ya mwezi Aprili , 2018 katika maeneo mengi yanayopata msimu mmoja wa mvua. Alisisitiza Dk. Kijazi.
Akizungumzia athari, alisema matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa yanatarajia kusababisha mafuriko katika maeneo machache, na pengine mlipuko wa magonjwa na uhaba wa maji safi na salama hivyo kushauri mamlaka husika kuchukua tahadhari kukabiliana na hali hiyo.
Pamoja na hayo ameishauri sekta ya afya kuchukua hatua stahiki kupunguza athari, na kuitaka menejimenti ya maafa na taasisi okozi kuchukua hatua katika utunzaji wa mazingira, matumizi sahihi ya ardhi na mipango miji.
"...Vyombo vya habri vinashauriwa kufuatilia kupata na kusambaza taarifa sahihi za mwenendo wa hali ya hewa ikiwemo tahadhari kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Aidha, vyombo vya habari vinashauriwa kushirikiana na wataalamu wa sekta husika katika kuandaa na kusambaza taarifa hizo za hali ya hewa kwa jamii," alisema Dk. Kijazi. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa utabiri wa mvua za msimu wa mwezi Novemba 2017 hadi mwezi Aprili 2018 ikiwa ni kwa mara ya kwanza TMA kutoa utabiri huo. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa utabiri wa mvua za msimu wa mwezi Novemba 2017 hadi mwezi Aprili 2018 ikiwa ni kwa mara ya kwanza TMA kutoa utabiri huo. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa utabiri wa mvua za msimu wa mwezi Novemba 2017 hadi mwezi Aprili 2018 ikiwa ni kwa mara ya kwanza TMA kutoa utabiri huo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)