Pages

KANDA YA ZIWA WAENDELEA KUJISHINDIA ZAWADI ZA 'MCHONGO CHINI YA KIZIBO' YA COCA-COLA

Washindi wa Mchongo chini ya kizibo ya Coca-Cola ya Mchongo chini ya kizibo wakifurahi na zawadi zao, wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika jijini Mwanza.
Washindi wa Mchongo chini ya kizibo ya Coca-Cola ya Mchongo chini ya kizibo wakifurahi na zawadi zao, wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika jijini Mwanza.
Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Cocacola mkoani Mwanza Samwel Makenge,(kushoto) akimkabidhi pikipiki Marysiana Kijita, baada ya kushinda promosheni ya ‘ Mchongo chini ya kizibo’ wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika jijini Mwanza.

Wakazi wa kanda ya ziwa na mikoa jirani mambo yanazidi kuwanyokea kutokana na kuendelea kujishindia zawadi za pikipiki,Televisheni bapa za kisasa ,fedha taslimu na zawadi nyinginezo kupitia promosheni ya Coca-Cola inayoendelea ijulikanayo kama ‘Mchongo chini ya kizibo’

Wiki iliyopita washindi wa pikipiki 6 walikabidhiwa zawadi zao sambamba na washindi 2 wa televisheni wakiwemo wengine wengi waliojishindia fedha taslimu na t-shirt kutoka kampuni ya Coca-Cola.

Waliokabidhiwa pikipiki ni Derick Magnus (Nyakato), Ismail Hamis (Magu), Joseph Mafuru (Mahina Mwanza) Pendo (Bariadi Mkoani Simiyu), Daniel Keheta (Mkolani),na Marysiana Kijita (Hungumalwa).Waliokabidhiwa televisheni ni Rhoda Joel, Marco Kitula.

Wakiongea kwa furaha baada ya kukabidhiwa zawadi zao washindi hao waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kubuni promosheni zenye lengo la kuinua maisha ya wateja wake “Nimefurahi kujishindia pikipiki kutoka Coca-Cola nitaitumia katika shughuli za biashara ili kuongeza kipato cha familia yangu”.Alisema Marysiana Kijita,kwa furaha.

Derick Magnus alisema kuwa amefurahi kujishindia zawadi ya pikipiki kupitia promosheni ya ‘Mchongo Chini ya Kizibo’na kudai kuwa itamrahisishia usafiri wake binafsi na familia yake “Chombo hiki kitarahisisha usafari katika shughuli zangu za ujasiriamali sambamba na usafiri kwa familia yangu”.Alisema.

Mmoja wa washindi wa televisheni,Marco Kitula ,alisema kuwa zawadi aliyojishindia imekuja kwa wakati mwafaka ambapo ataweza kuona matukio mengi na michezo mbalimbali kupitia televisheni yake ya kisasa aliyojishindia “Napenda sana kuangalia matukio kupitia luninga na michezo mbalimbali nitaburudika vizuri na familia na marafiki”.Alisema kwa furaha.

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika kiwanda cha Nyanza mwishoni mwa wiki ,Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Japhet Kisusi,amesema kuwa promosheni hii ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuboresha maisha ya wateja wanaotumia bidhaa za kampuni inaendelea vizuri na washindi wanaendelea kukabidhiwa zawadi zao.

Aliwataka wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa kuendelea kuchangamkia promosheni kupitia kunywa soda za kampuni ya Coca-Cola na kuongeza kuwa zawadi bado ziko nyingi.”Mchongo Chini ya Kizibo inawezesha kujishindia zawadi nono za fedha taslimu,bodaboda,televisheni aina ya SONY LED,kofia na soda za bure.

Alisisitiza kuwa ili mteja kujishindia zawadi anatakiwa kubandua kiambatanisho laini kilichopo chini ya kizibo cha soda. Kwa upande wa fedha taslimu kuna zawadi za shilingi 5,000/-, 10,000/- na 100,000 “Kwa upande wa zawadi ya bodaboda anachotakiwa kufanya mteja ni kukusanya vizibo vitatu vyenye picha zinazokamilisha picha ya bodaboda – kuonyesha upande wa Nyuma, Katikati na Mbele na zawadi nyinginezo za Televisheni, kofia, T-shirt na soda za bure zinapatikana chini ya kiambatanisho laini chini ya kizibo kama zilivyo zawadi kubwa’’.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)