Pages

WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KISOMO,JIJINI DAR

Wanajopo walioshiriki mjadala huo kutoka kushoto ni Viola Julius mratibu wa tovuti ya iSwapMyBooks, Given Edward toka mtandao wa MyElimu,Kiya JK wa taasisi ya
SEMA na  Irene Kiwia wa
TWA network
Mmoja wa wachangiaji Bw. Yeriko Nyerere  akichangia jambo wakati wa siku hiyo
 Bw. Paschal Masalu kutoka Elimika Wikiendi akiendelea ku Tweet wakati wa Siku hiyo ya kisomo
Baadhi ya wadau mbalimbali wa Elimu wakiwa katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kisomo

Wadau mbalimbali wa elimu wamekutana kuadhimisha siku ya kimataifa ya
kisomo ambayo hufanyika Septemba 8 kila mwaka. Maadhimisho hayo
yaliyoandaliwa na taasisi ya iSwapMyBooks kwa kushirikiana na SOMA pia
Elimika Wikiendi ulihusisha mjadala wa namna ambavyo Tanzania inaweza
kutumia faida ya uwepo wa nyenzo za kidigitali katika kusaidia watoto na
watu wazima kujifunza.












Akifungua maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji
wa taasisi ya SOMA Bi. Demere Kitunga alieleza namna ambavyo kwa miaka ya
karibuni Tanzania imekuwa ikipiga hatua katika matumizi ya nyenzo za
kiditali kutokana na usambaaji wa matumizi ya vifaa vilivyounganishwa na
mtandao wa intaneti hivyo kupelekea uhitaji katika kutumia nyenzo hizi
katika kuboresha namna ambavyo watoto wanaweza kujifunza masomo.



Wanajopo walioshiriki mjadala huo Irene Kiwia wa
TWA network, Given Edward toka mtandao wa MyElimu, Kiya JK wa taasisi ya
SEMA na Viola Julius mratibu wa tovuti ya iSwapMyBooks walielezea namna
ambavyo taasisi zao zimekuwa zikitumia njia za kidigitali kuwahamasisha
watoto na vijana  kujifunza kwa kubadilishana ujuzi kupitia mtandaoni.



Washiriki wengine kwa namna tofauti walionyesha
wasiwasi kwa namna ambavyo utaratibu wa watu kujisomea unaendelea
kutoweka na hasa kwa wazazi ambao wamekuwa hawana utaratibu wa
kuwanunulia watoto vitabu badala yake kuwapa simu za mkononi ambazo
wamekuwa wakizitumia kwa mambo yasiyofaa. Akijibu wasiwasi huo,
Mkurugenzi wa taasisi ya SEMA ndugu Kiiya JK alisema ni wakati mitaala
ya masomo ibadilike kuendana na hali halisi. “Tunalazimika kama
Watanzania kutengeneza vitabu vinavyoendana na hali halisi ya maisha
yetu kwa sasa, wenzetu wamegundua hilo na wamekuwa mstari wa mbele
kuwekeza katika kuchapisha vitu vinavyowafaa watoto wetu”.



Siku ya kimataifa ya kisomo ilianzishwa na
shirika la UNESCO miaka 50 iliyopita ambapo kaulimbiu ya mwaka huu
ilikuwa “Kisomo Katika Ulimwengu wa Kidigitali”.


No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)