Pages

Airtel TImiza yafaidisha wajasiriamali zaidi nchini.

•  Asilimia 80 ya wateja wa Airtel money 80% wanufaikana nikopo rasmi    
•   Asilimia 50 ya watanzania sasa wapata huduma za kifedha kupitia simu zao za mkononi            
DAR ES SALAAM,  11 Septemba 2017 – Airtel Money imetangaza kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wateja wake sasa wanaweza kupata mikopo rasmi kwa kupitia Airtel Timiza ambayo ni huduma ya mikopo kwa wajasiriamali.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw, Sunil Colaso alisema huduma hiyo, iliyozinduliwa Novemba 2014, kwa sasa inatoa mikopo takriban 10,000 nchi nzima kwa siku.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, asilimia 80 ya wateja wa Airtel Money hawakuwa wamewahi kupata mkopo rasmi, hii ikiwa ni dalili kuwa watanzania wengi zaidi sasa hivi wanapata huduma za kifedha kwa mfumo wa kidijitali.
“Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa asilimia 25 ya mikopo inatumika katika kuongeza mitaji na pia kuimarisha dhamana. Inatia moyo kuona jinsi wateja wetu wameweza kupata huduma za kifedha kupitia Airtel Money,” alisema.
Alisema Airtel Money imejidhatiti kuhakikisha watu wengi zaidi wanapata huduma za kisasa ambazo zinasaidia kukuza biashara. “Biashara ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania hivi ni muhimu kuwezesha sekta hii,” alisema.
Alisema kabla ya Airtel Timiza, watanzania wengi walikuwa wanakopeshana fedha kwa mifumo isiyo rasmi kwa kupitia ndugu na jamaa au hata njia nyingine ambazo sio salama.
“Leo hii Airtel Timiza inatoa mikopo kwa njia ambazo ni salama zaidi kwani wafanyabiashara mbalimbali wanaweza kupokea mikopo hata bila kuwa na akaunti ya benki au dhamana.  
Alisema kwa sasa asilimia 50 ya watanzania wanaweza kupokea huduma za kifedha kwa kupitia simu zao.
Grace, ambaye ni mfanyabiashara wa mashuka kutoka Dar es Salaam, alisema kwa sasa anaweza kutimiza mahitaji ya wateja wake kwani Airtel Timiza imemuwezesha kununua mzigo zaidi na kulipa mkopo baada ya kufanya mauzo.
“Kabla ya Airtel Timiza nilikuwa napata shida ya kuweka oda kubwa kwa sababu ya ukosefu wa mtaji wa kutosha lakini huduma hii imenisaidia kukuza biashara yangu na ninaweza sasa kuchangia katika ujenzi wa nyumba yetu hapa Dar es Salaam,” alisema.
Airtel Money inafanya kazi na JUMO, ambayo ni kampuni ya teknolojia inayohakikisha wateja wanapokea huduma bora zaidi za Airtel Timiza. JUMO ina uwezo wa kuangalia matumizi ya mteja ya simu na kupendekeza kiasi cha mkopo anachostahili kupata na pia kupendekeza bidhaa zinazomfaa mteja na masharti.  
Pamoja na kuhakikisha kila mteja anafikiwa na huduma za mikopo, Airtel Money imeweka kipa umbele kwa kuhakikisha wateja wanapata mikopo wanayostahili, kuboresha na kutanua mtandao wa mawakala.
Hadi kufikia Disemba 2016, kulikuwa na akaunti milioni 18 za miamala ya simu zilizosajiliwa (Ripoti ya Robo mwaka ya TCRA kuhusu takwimu za mawasiliano, Disemba 2016). Katika ukanda wa sahara ya Afrika, kuna akaunti milioni 277 za miamala ya simu zilizosajiliwa katika ukanda huo ambayo ni idadi kubwa kushinda idadi ya akaunti za benki kama ilivyoripotiwa na GSMA.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)