Sehemu ya Darasa la Vijana wa Shule za Msingi kutoka sehemu mbalimbali.
Meneja Mradi wa Aitel & DTBI Computer Lab, Agape Jengela akizungumzia kuhusu mradi huo wa Airtel Fursa ambao umenza na Darasa la Vijana wa Shule za Msingi kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam, katika fursa hiyo Watoto wamejifunza kutengeneza ROBBOT.
Kampuni yasimu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) imeanza kutoa mafunzo ya Tehama kesho katika maabara ya kompyuta iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama na kuwawezesha vijana zaidi ya 20 waliojiandikisha kuanza kupata mafunzo hayo
Mafunzo hayo yameanza kufatia Airtel na DTBi kutangaza kuanza kwa mafunzo hayo na kuwaalika vijana kuanzia ngazi ya shule za msingi,sekondari, vyuo vikuu na wafanya biashara kujiandikisha na kufaidika na mafunzo haya yatakayowasaidia kuvumbua application mbalimbali, kuwapatia vijana ujuzi katika mswala ya Tehama na pia kuwawezesha vijana wajasiriamali kuendesha shughuli zao za kibiashara kwa kutumia technologia za kisasa
Akiongea kuhusu kuanza kwa mafunzo hayo, Meneja Mradi wa Airtel Bi Jane Matinde alisema, Tumefurahishwa sana na muitikio mkubwa uliofanya na vijana hususani wa shule hii ya msingi ya kijitonyama na watoto kutoka maeneo mengine katika kujiandikisha na kuanza mafunzo haya. Tayari tunao jumla ya wanafunzi 20 ambapo wamejipanga kuanza kujifunza kesho kuanzia saa 9 mchana hadi saa 11 jioni. Tunaamini hii ni fursa muhimu sana kwa vijana wetu wenye kuonyesha dhamira yao ya kubobea katika maswala ya Tehama na komputa ya sayansi kuanza sasa wakiwa katika umri mdogo.
Bado tunapokea maombi ya kujiunga hivyo tunatoa wito kwa vijana wa sekondari , wale waliomaliza darasa la saba , wafanyabiashara kutumia vyema maabara hii yenye lengo la kuwezesha jamii hususani vijana kuongeza ujuzi na ueledi kwenye maswala ya technologia na Tehama kwa ujumla.
Kwa upande wake Meneja wa maabara ya Airtel Fursa , Agape Jengela alisema “ Tayari tumejipanga kutoa mafunzo kwa vijana, walimu wamejipanga vyema katika kuhaikisha vijana hawa wanapata mafunzo bora. Mafunzo hayo ni pamoja na lego Robotics, program za uhuishaji kwa watoto(ziitwazo scratch) na ubunifu na uchapishaji wa“3D objects” msingi wa kompyuta, uelewa wa kompyuta, kutengeneza program mbali mbali
Bado tunapokea maombi, Tunato wito kwa wazazi na walezi kuwaandikisha vijana wao kwa kupitia www.teknohama.or.tz na www.a irtelfursa.com au kwa kutembelea maabara iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)