Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO katika Siku ya Kimataifa ya Ufikivu Habari Sept 28 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO katika Siku ya Kimataifa ya Ufikivu Habari Sept 28

Katika ulimwengu wa uchangamano, ufikivu wa habari ni muhimu katika kujenga jamii yenye maarifa, iliyo shirikishi na endelevu. Huu ndio ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Ufikivu Habari kwa Wote (IDUAI), ukizingatia jukumu muhimu ambalo ufukivu wa habari hufanya katika kuendeleza Agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu.

Ufikivu habari ni haki ya msingi. Inawawezesha wanawake na wanaume kuelewana kushiriki katika kujenga na kushirikiana ujuzi wanaohitaji ili watoe mchango kikamilifu katika jamii yao. Raia wenye taarifa sahihi huifanya serikali iwajibike. Ufikivu Habari ni dereva wa uvumbuzi na ubunifu, kuongeza fursa kwa wote, hasa kwa wasichana na wanawake.

Ufikivu habari huanza na kujitolea kwa Serikali kutengeneza, kueneza na
kutekeleza sera na sheria zinazohusu haki ya habari na kuhakikisha kuheshimiwa kwa haki hii ya kibinadamu. Hii inahitaji utaratibu wa ufanisi wa utekelezaji na utamaduni wa uwazi katika aina zote za taasisi. Wananchi wanahitaji pia kuwa na fikra pana, ujuzi wa kusoma na ujuzi wa kidigitali ambao unahitajika kufikia, kuchambua na kutumia habari kwa njia tofauti, nje na ndani ya mitandao. Hii ndiyo maana UNESCO inaziomba serikali zote na washirika kutumia uwezo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili kusaidia kufikia Lengo la 4, Elimu Endelevu inayolenga kuhakikisha "elimu shirikishi, sawa na ya ubora na kukuza fursa za elimu isiyo na mwisho kwa wote; Ufikivu wa Habari pia unajumuisha kukuza uandaaji wa maudhui yanayofaa, yenye kulenga jamii husika na yanayopatikana kwa lugha mbalimbali. Yote hii inahitaji sera zenye ufanisi na ushirikiano mzuri katika ngazi zote.
Siku ya Kimataifa ya Ufikivu Habari kwa Wote pia ni fursa ya kurejea ahadi yetu ya uhuru wa kujieleza na usalama wa waandishi wa habari. Vyombo vya habari huchukua nafasi muhimu katika kuwezesha ufikivu wa habari kwa wananchi na katika kufuatilia masuala muhimu ya kijamii na wakati huo huo vikiwaelimisha wafuatiliaji kwa kuwapa ufahamu na ujuzi. Haiwezekani kuwepo kwa ufikivu wa habari kwa wote bila kuwepo kwa vyombo vya habari vilivyo huru.

Ufikivu wa habari sio tu ni lengo peke yake; pia ni mchangiaji muhimu katika
utekelezaji wa malengo mengine yote ya Maendeleo Endelevu. Kwa hiyo ni
muhimu tuendeleze juhudi zetu ili kuhakikisha kuwa kila mwanamke na mwanamume wanafurahia ufikivu kamili wa habari.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages