KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA NA MAENDELEO YA JAMII,SIHABA NKINGA AFUNGUA MKUTANO WA REPSSI JIJINI ARUSHA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA NA MAENDELEO YA JAMII,SIHABA NKINGA AFUNGUA MKUTANO WA REPSSI JIJINI ARUSHA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Watoto,Bi  Sihaba Nkinga akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa watoto  ulioandaliwa na taasisi ya REPSSI yenye makao yake nchini Afrika Kusini  kutoka mataifa zaidi ya 30 barani Afrika unaofanyika jijini Arusha,mkutano huo pamoja na mambo mengine unalenga kuwawezesha  watoto  sauti zao kusikika na kuwajenga kisaikolojia

Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi ya REPSSI,Noreen Huni ambaye ni raia wa
Zimbabwe akizungumza katika mkutano huo wa kimataifa jijini Arusha leo.

Watoto kutoka mataifa mbalimbali wakifatilia mada kwenye mkutano huo.


Watoto kutoka mataifa mbalimbali wakiwa kwenye mkutano  ambao unawapa fursa ya kuwasilisha taarifa za matukio ambayo ni changamoto kwao.

Watoto wakiwa kwenye mkutano ambao unawapa fursa ya kuwasilisha taarifa za matukio ambayo ni  changamoto kwa mamlaka husika na kutafutiwa ufumbuzi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya  Jamii,Jinsia,Wanawake na Watoto,Bi Sihaba Nkinga(katikati) akiwa katika  picha ya pamoja na Mwenyekiti wa baraza la watoto nchini,Joel vFesto(kushoto) na Mwenyekiti wa baraza la watoto nchini Kenya,Brian Musyoka  katika mkutano wa kimataifa wa watoto ulioandaliwa na taasisi ya REPSSI yenye makao yake nchini Afrika Kusini .

Mmoja wa washiriki akifatilia kwa makini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya  Jamii,Jinsia,Wanawake na Watoto,Bi Sihaba Nkinga(katikati)akiagana na  viongozi wa watoto mara baada ya kufungua mkutano huo jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages