Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akisalimiana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro (ACP) Hamisi Issah, na anayeshuhudia katikati ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (DCP) Charles Mkumbo, alipowasili mkoani Arusha, kuwapa pole askari wa jeshi hilo kufuatia ajali ya moto iliyoteketeza makazi yao waliyokuwa wakiishi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiangalia eneo lililoathiriwa na ajali ya moto iliyoteketeza makazi ya askari tukio lililotokea jana majira ya jioni, IGP Sirro yupo mkoani Arusha, kwa ajili ya kuwapa pole askari na familia zao pamoja na salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, na kutoa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 260 kwa ajili ya kujenga upya makazi yao kulia ni kamanda wa Polisi mkoani humo (DCP) Charles Mkumbo
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kulia), akiwa ameongozana na Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, alipowasili mkoani humo kwa ajili ya kuwapa
pole askari na familia zao kufuatia ajali ya moto iliyoteketeza makazi yao
waliyokuwa wakiishi pamoja na kuwapa salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John
Magufuli, na kutoa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 260 kwa ajili ya kujenga
upya makazi yao. Picha na Jeshi la
Polisi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)