Meneja Miradi Airtel Tanzania Jane
Matinde akizungumza wakati wa semina kwa vijana kuhusu umuhimu wa kusoma kwa
kutumia mtandao kupitia aplikesheni ya VISOMO inayotumiwa na VETA kwa
kushirikiana na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel iliyofanyika makao makuu
ya kampuni hiyo Morocco, Dar es Salaam jana.
Baadhi ya washiriki wa semina kwa
vijana kuhusu umuhimu wa kusoma kwa kutumia mtandao kupitia aplikesheni ya
VISOMO inayotumiwa na VETA kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
wakifuatilia kwa umakini mafunzo yaliokuwa yanatolewa kwa ajili ya
kuwahamamisha jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Magilatech Company Ltd. Godfrey Magila na mtaalamu wa tenklojia
akitoa mafunzo kwa vijana
waliodhuria semina kuhusu umuhimu wa kusoma kwa kutumia mtandao kupitia
aplikesheni ya VISOMO inayotumiwa na VETA kwa kushirikiana na Kampuni ya simu
za mkononi ya Airtel iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Morocco, Dar es
Salaam jana.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikia na VETA leo wametoa mafunzo kwa
vijana mkoani Dar itakayowawezesha kuongeza ujuzi na kuenda sambamba namahitaji
ya soka la ajira na kujiajiri.
Mafunzo
hayo yenye lengo la kutoa fursa mbalimbali zinazopatikana kupitia ushirika wa
watoa huduma hao yanalenga katika kuwawezesha vijana nchnini kujiendeleza
kielimu kupitia application ya VSOMO kwa kupata masomo ya ufundi stadi ya VETA
kupitia simu zao za mkononi ili kuongeza ujuzi wao
Akiongea
wakati wa semina hiyo , Meneja Mradi wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema
Tumeonelea vyema kufanya semina hii ili kuongeza uelewa kwa vijana juu ya
fursa hii muhimuinayotoa nafasi ya kijana kujitambua na kujiajiri mwenyewe mara
baada ya kusoma masomo ya Ufundi kupitia simu zao za mkononi na kupata
cheti. Tunao vijana Zaidi ya wateja 30,000 ambao wamepakua application ya
VSOMO kati yao 9,000 wamejiandikisha ili kusoma kwa mtandao lakini idadi ya waliopata
vyeti bado ni chache, hivyo tumeonelea ni vyema kujikita katika kutoa elimu na
kuwahamashisha watanzania kutumia technologia hizi za kisasa kujisomea wakati
wowote mahali popote kupitia simu zao za smartphone na hatimae kufanya mafunzo
ya vitendo na kupata cheti
Tunatoa
wito kwa watanzania hususani vijana kuchangamkia fursa hii kwa kupakua
application ya VSOMO kwenye simu zao na kusoma kozi hizi za ufundi ambazo
gharama yake ni 120,000/= hadi kumaliza na kupata cheti.
Kwa
upande wake mtaaalamu wa technologia na Mkurugenzi wa Magilatech Company Ltd.
Bw, Godfrey Magila alisema, Techonologia inakuwa kwa kasi sana ni muhimu
kutumia Tehama katika kuleta tija katika kibiashara, kilimo , elimu na
kadhalika. Kwa kuona hivyo tumeanzisha hii application ya VSOMO ambayo ni ya
kwanza dunia kutoa mafunzo ya ufundi kupitia simu na Tanzania tunajivyunia
kupiga hiyo muhimu.
Naye
Meneja Mradi wa VSOMO VETA , Bwana Charles Mapuli alisema, Ushirikiano wetu na
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kunaongeza wito katika kutoa elimu ya
ufundi na kuwafikia watanzania wengi Zaidi. Napenda kuwahakikishia kuwa masomo
haya ya VETA kupitia simu yamehakikiwa na VETA kuhakikisha yanatolewa katika
ubora na viwango vinavyotakiwa, na hivyo natoa wito kwa watanzania kutumia
fursa hii kujiendeleza. Lengo letu ni kuhakikisha kila mtanzania anapata
fursa ya kujiendeleza na kuwa na ueledi utakaomuwezesha kuajiriwa au
kujiajiri.
Kozi
zinazopatikana katika application ya VSOMO ni pamoja ni Huduma ya chakula
na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta,umeme wa viwandani,
ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme wa magari. Vilevile Ufundi umeme wa
manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi
Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)