Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Luckiness Amlima akisisitiza jambo katika maandalizi ya Mbio za hisani za Namtumbo Selous Marathon ambazo zinatarajia kufunguliwa rasmi tarehe 30, Septermber 2017
Aliyekaa katikati ni mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Luckiness Amlima ,kusho kwake ni Afisa mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzania Khadija Pallangyo na kulia kwake ni Diwani wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Judith Mbogoro.
Baadhi ya waandishi wa vyombo vya habari mkoani Ruvuma wakifuatilia taarifa ya mgeni rasmi juu Mbio za hisani za Namtumbo Selous Marathon ambazo zinatarajia kufunguliwa rasmi tarehe 30, Septermber 2017 .
Kusho kwako ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Luckiness Amlima akielekezwa jambo na Afisa mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzania Khadija Pallangyo.
Baadhi ya waandishi wa vyombo vya habari mkoani Ruvuma wakifatilia taarifa ya mgeni rasim juu Mbio za hisani za Namtumbo Selous marathon ambazo zinatarajia kufunguliwa rasmi tarehe 30, Septermber 2017 .
……………….
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Ruvuma TV Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Luckiness Amlima, amesema mbio hizo ni maalum ambazo zinalenga kukukusanya pesa kutoka kwa watu wote wanaounga mkono na wanao Itakia heri wilaya ya Namtumbo katika kuboresha afya ya wana Namtumbo na kuongeza umri wa kuishi wa Tanzania kwa kufanya maisha yao yawe salama zaidi na yenye ubora stahiki kwani Afya njema ni nguzo ya furaha na tija.
“ Wote tunajua kuwa Tanzania inaelekea kwenye ustawi zaidi na nchi ya uchumi wa kati . Kwa mantiki hii, uboreshaji wa huduma za afya ni za umuhimu mkubwa na wa kupewa kipaumbele, Tukiwa na lengo hili zuri sisi wana Namtumbo tumetafuta marafiki wanaotuunga mkono.– Mantra kampuni tanzu ya uchimbaji madini ya Uranium One na ROSATOM, Kampuni ya Nguvu za Nuklia ya Urusi, tumeamua kuandaa mbio za marathon zenye lengo la kukusanya pesa takriban Shs Bilioni 1.2 kutoka kwa wadau mbalimbali ambazo zote zitatumika kukamilisha hospitali ya wilaya ya Namtumbo” Amesema mkuu wa wilaya hiyo.
Mbio hizi au Marathon zitahusisha mbio za 21 km/nusu marathon , 5-km na 2.5 km kwa kuzingatia umri, jinsia na watu tofauti kama walemavu.
Kwa washiriki watakao shinda watapatiwa zawadi mbali mbali zikiwemo Simu, Tv na pesa tasilim pamoja na zawadi kutoka nchini Urusi. Gharama za ushiriki kwa watanzania kwa KM 21 itakuwa shilingi elfu kumi, km 5 itakuwa shilingi elfu saba na miatano , km 2.5 itakuwa shilingi elfu 5 na kwa wageni ( Wasio wa Tanzania ) dola 25 na kama mshiriki anadhaminiwa na shirika atatoa shilingi laki moja.
Mbio hizo za hisani zinaongozwa na kauli mbiu inayosema PAMOJA TUNAWEZA/TOGETHER WE CAN ambapo mkuu wa wilaya ya Namtumbo Luckiness Amlima amewaomba wananchi na wadau kushiriki mbio hizo kikamilifu ili kufikia malengo vile vile ametoa rai kwa viongozi wa ngazi mbali mbali za serikali kutoa ushirikiano.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)